Jeshi la Polisi #Tanzania limewafikisha Mahakama ya Kibaha Watu saba wakituhumiwa Kuhujumu Uchumi kwa kukutwa wakisafirisha vyuma chakavu vikiwemo vyuma vilivyoibiwa kwenye Reli
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Richard Boaz amesema, miongoni mwa Watuhumiwa waliofikishwa Mahakamani ni pamoja na Mawakala na Wafanyabiashara wenye Viwanda vya Kuchakata Vyuma Chakavu
Boaz amesema, Serikali inatumia fedha nyingi kuimarisha miundombinu ikiwemo ya Reli lakini baadhi ya watu wasio wema na wenye uchu wa mali wamekuwa wakihujumu jitihada hizo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments