WAZIRI MKUU MAJALIWA, SPIKA NA MO DEWJI KUHUDHURIA HAFLA YA KUWAKARIBISHA WABUNGE | ZamotoHabari.


Charles James, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ni miongoni mwa wageni wa heshima watakaohudhuria hafla ya kuwakaribisha wabunge wapya ambayo imeandaliaa na Wabunge wanachama wa Klabu ya Simba tawi la Bunge jijini Dodoma.

Hafla hiyo pia itahudhuriwa na Spika wa Bunge na Naibu Spika ambao ni wanachama wa Simba pamoja na mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Timu hiyo, Mohammed Dewji 'Mo'.

Akizungumzia hafla hiyo, Mwenyekiti wa Tawi la Simba Mjengoni na Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi amesema lengo la hafla hiyo itakayofanyika kesho jijini Dodoma ni kula chakula cha usiku pamoja, kufahamiana pamoja na wabunge wapya kupata fursa ya kujisajili kwenye tawi hilo na kujisajili na kadi ya uanachama ya Timu hiyo.

Shangazi amesema lengo la kuanzishwa kwa tawi hilo ni kuuza bidhaa za klabu hiyo na kuwa wakala wa bidhaa na vifaa vya Simba pamoja na kupata sehemu mahususi ya wabunge kutazama mpira.

" Alichokisema Mwenyekiti Mo Dewji kwamba watanzani wengi ni Simba wala hakukosea, mfano hapa Bungeni wabunge wa zamani na wa sasa ambao wamejisajili Simba ni 280 unaweza ukaona namna gani tulivyo wengi.

Simba ni muongoza mwendo tutaeleza mipango kabambe tuliyonayo, lengo letu ni kulifanya tawi letu kuwa kubwa zaidi duniani, ni Bunge la Tanzania tu ambapo klabu ya mpira ina tawi ndani yake na klabu hiyo ni Simba pekee, wengine wakianzisha basi wamechukua kwetu," Amesema Shangazi.

Mwenyekiti wa Tawi la Simba Mjengoni ambalo linaundwa na Wabunge Wanachama wa Klabu ya Simba, Rashid Shangazi akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.
Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Tawi la Simba Mjengoni, Rashid Shangazi.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini