Zari Athibitisha Kuachana na Aliyekuwa Akimtangaza Kama Mpenzi Wake Aliyemtambulisha Kama "King Bae" | ZamotoHabari.


Mrembo na Mwanamama @zarithebosslady amethibitisha kuachana na mwanaume wake aliyemtambulisha mtandaoni kama ‘King Bae’ ambaye alifikia hadi hatua ya kumvisha pete ya uchumba.


Ikumbukwe, mara baada ya #Zari kuachana na #Diamond Februari mwaka 2018, na hii ni baada ya #Zari kutangaza jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kwamba msanii huyo amekuwa akimsaliti kwa kuwa na wanawake wengine, #Zari alikaa kwa muda kidogo ndipo akaweka wazi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume huyo ambaye hakuwahi kumuonyesha Sura.


Akizungumza na Wasafi TV mwishoni mwa Wikiendi, #Zari amesema kuwa ni kweli mwanaume huyo alikuwepo na wala haikuwa kiki lakini kuna vitu kati yao vilitokea hadi kupelelea mahusiano yao kuvunjika.


Kwa takribani wiki moja sasa #Zari amekuwa kwenye headsline upande wa stori za burudani hapa nchini kutokana na ujio wake na watoto wake, #Tiffah na #Nillan aliowaleta kumuona baba yao mzazi, msanii Nasib Abdul @diamondplatnumz.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini