Zijue dalili za awali za ugonjwa wa kisukari | ZamotoHabari.




Ili kuweza kutambua kama umeugua ugonjwa wa kisukari unatakiwa kujua dalili za awali za ugonjwa huo ambazo ni; 

1. Kukojoa mara kwa mara. 
Ugonjwa wa Kisukari unasababisha sukari kutolewa kwenye njia ya mkojo. Sukari inapotolewa  huambatana na maji hivyo  kukufanya upate mkojo kila mara. 

2. Kuhisi Kiu mara kwa mara. 
Unapokuwa na kisukari unapoteza maji mengi kwenye mkojo hali hii husababisha kupata koi mara kwa mara. 

3. Kusikia njaa kali kila mara. 
Mwili unapoteza uwezo wa kutumia sukari katika kazi zake. Hali hii hufanya mwili wako kuhisi kuwa hakuna chakula cha kutosha. Hii ndio sababu inakufanya  kuhisi njaa kila mara na hata baada ya kula unaendelea kuhisi njaa. 

4.Uchovu wa mwili 
Hii hutokana na mwili kushindwa kutumia  sukari  kutengeneza nishati ya kuwezesha mwili kufanya  kazi zake. 

5.Kupoteza uzito/Kukonda 
Ugonjwa wa Kisukari hupunguza uwezo  wa mwili kuhifadhi sukari kwenye misuli. Hivyo mwili wako utaanza  kupoteza uzito na kuanza kukonda.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini