BHALLO ATOA SOMO KWA SINGLE MOTHER'S | ZamotoHabari.








EJAZ Bhallo mtunzi na Mwanahistoria ameshiriki na kutoa hotuba katika  Semina ya "Single Mother's" iliyoandaliwa na "Save The Society." Ambapo alizungumza juu ya, "mambo mawili ya muhimu ili kufikia malengo," Pia, alikuwa mmoja ya  wadhamini wa hafla hiyo.

Kongamano hilo liliwashirikisha "Single Mothers" kutoka sehemu na maeneo mbalimbali nchini Tanzania huku madhumuni ya Semina hii ilikuwa ni kuwaelimisha washiriki kwenye mambo mbalimbali ikiwemo Afya ya Akili, usimamizi wa fedha, sanaa ya uzungumzaji na Ujasiriamali.
 
Semina hii pia iliwajumuisha wasemaji wengine mashuhuri nchini Tanzania wakiwemo  Harris Kapiga (mwandishi wa habari,) Bi. Faiza Ally (Mjasiriamali,) Rodrick Nabe (Mwandishi,) Mr. Bright Motivation (Mhamasishaji,)Selina Condrady (MC) na  Dk.Martha Kungu (Mwanasaikolojia na Mwanzilishi wa @afya_passion.)
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini