BODI YA UTALII TANZANIA YASAINI MKATABA WA MAELEWANO NA CI GROUP | ZamotoHabari.

 BODI ya utalii nchini (TTB) yasaini makubaliano na Kampuni ya CI Group kwa ajili ya kutangaza Utalii wa ndani.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini Devotha Mdachi amesema Bodi itaendelea kutoa ushirikiano kwa watu ambao kidhati wataendelea kutangaza Utalii.

"Kumekuwepo mbinu nyingi zinazotumika kutangaza Utalii, kumekua na Kampeni pamoja na kutumia watu maarufu katika kutangaza Utalii wetu na vivutio vili opo nchini kwani Utalii ni mojawapo ya sekta ambayo inaongeza pato la taifa mara baada ya watalii wanapotembelea vivutio vyetu."

Mdachi amewapongeza sana Kampuni hiyo ambayo imeonyesha dhamira ya dhati kutangaza Utalii kupitia sanaa za sarakasi.

"Kupitia sekta ya Utalii wanufaika watakuwa watu wengi kwani wataweza kutapata fursa mbalimbali kupitia majukwaa hayo ya Sanaa."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya kutangaza Utalii (CI  GROUP) Constantine Magavika ameishukuru Bodi ya Utalii kupitia Wizara Maliasili na Utalii.

"Tutatumia fursa hii tulipewa na Bodi ili kuonyesha kwa kiasi gani tutaweza kuitangaza Sekta ya Utalii nje na ndani ya nchi kupitia onyesho la Sarakasi la Mama Afrika linalotarajia kufanyika Disemba 23 mwaka huu katika viwanja vya jeshi Masaki Jijini Dar es salaam."

Aidha, Magavika ameeleza dhamira ya kuandaa onyesho hilo ni kuwapa fursa wakina Mama ambao wanafanya Sarakasi nchini pamoja na bidhaa za kitamaduni ya Kitanzania, Vyakula pamoja na  Mavazi.Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Devotha  Mdachi(kulia) akikabidhiana Mikataba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kutangaza Utalii (CI group) mara baada ya kusaini Mkataba wamakubaliano hayo.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini