Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya mkoa huo, Dk. Binilith Mahenge akiongoza kikao cha Bodi ya Barabara ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe walipata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa barabara mkoani humo kutoka Tanroad na Tarura Desemba 16, 2020 jijini Dodoma.
Dk. Mahenge amezitaka Tarura na Tanroads kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika kwa kupata maoni na ushauri wao kabla ya kuanza ujenzi wa barabara na madaraja katika maeneo yao ili kujenga miradi imara inayozingatia jiongrafia na historia ya eneo husika.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula akisoma ajenda za kikao hicho.
Spika wa Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai akitoa hoja kuhusu umuhimu wa Miji midogo kama Kibaigwa kutengewa na Tanroads fedha za ujenzi wa barabara na kupanua maeneo ya kuegesha magari yakiwemo malori ili kupanua wigo wa kibiashara na kuongeza ajira kwa vijana katika eneo hilo. Ndugai pia ni mjumbe wa bodi hiyo.
Mratibu wa Wakala wa Barabara vijijini (TARURA) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe akitoa taarifa kwenye kikao hicho kuhusu mipango ya utekelezaji ya miradi ya barabara za Tarura kufikia hadi Novemba, 2020.
Mhandisi Mwandamizi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Mhandisi Jacob Mukasa akielezea katika kikao hicho , kuhusu manufaa na namna mfuko unavyopanga vipaumbele vya kutoa fedha.
Mhandisi wa Barabara wa Tanroads, Clement Ngirwa akielezea katika kikao hicho, kuhusu utaratibu wa kupandisha hadhi barabara na majukumu ya Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara katika Hadhi Stashiki.
Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde akichangia hoja akitaka uwepo utaratibu wa barabara za jamii nazo kutengea fedha kwa ajili ya matengeezo.
Mbunge wa Kondoa Vijijini, Dk. Ashatu Kijaji akichangia hoja wakati wa kikao hicho kwa kuzitaka Tarura na Tanroads kuwa na watalaamu wenye ueledi ili waweze kujenga miradi imara kuiiko wanaojenga miradi ya barabara na madaraja dhaifu ambayo mvua ikinyesha inabomoka kirahisi.
Mbunge wa Chemba, Mohamed Monni, akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota akichangia hoja wakati wa kikao hicho. Kuhoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dk. Fatuma Mganga na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda.
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao hichoKaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Salome Kabunda akitoa taarifa kwenye kikao hicho kuhusu mipango ya utekelezaji ya miradi ya barabara za Tanroads hadi Novemba, 2020.
wenyekiti wa Halmashauri ya Chemba, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi hiyo, Sambala Said
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments