DONALD TRUMP, RAIS KINARA KWA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII | ZamotoHabari.

 


*Achapisha mara 18 kwa siku katika ukurasa wake wa Twitter.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IKIWA zimebaki siku chache kwa Rais wa Marekani Donald Trump kumwachia ofisini Rais mteule wa taifa hilo Joe Biden, Trump ametajwa kuwa kiongozi kinara wa kutumia mitandao ya kijamii hasa Twitter na Instagram katika kutoa taarifa za kiofisi.

Ikumbukwe kuwa Donald Trump ameongoza kwa kipindi kimoja pekee kabla ya kushindwa  kung'ara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mapema Novemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa Shirika la utangazaji la kimataifa la CNN, imeelezwa kuwa Trump amekuwa Kinara wa kutumia mitandao ya kijamii na tangu akabidhiwe ofisini Januari 2017 kupitia ukurasa wa Twitter wenye wafuasi milioni 88.6 amechapisha maandiko mara 25,000 huku kwa siku moja akichapisha mara 18 na muda aliopumzika bila kuweka ujumbe Twitter  ni siku 1.9 kwa mwezi juni  2017 pekee.

Licha ya hayo Trump ameelezwa kukiuka taratibu za kiuongozi kwa kuendelea kutumia simu binafsi katika shughuli za kiofisi licha ya kuonywa na viongozi wa usalama na amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa zisizo za kweli na za kibaguzi na hadi kufikia Desemba 17, Twitter ilifuta machapisho 362 katika ukurasa wake wa Twitter.

Aidha Trump ameendelea kulaumiwa  kwa kushindwa kudhibiti mlipuko wa virusi vya Corona vilivyosababisha vifo 300,000 hadi kufikia Desemba 17 na waathirika milioni 17.

Imeelezwa kuwa tangu akabidhiwe Ofisi Trump ametembelea miradi yake mara nyingi zaidi hata wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona.

Imeelezwa Trump ametumia asilimia 21 ya siku zake akiwa Rais kutembelea mradi wake wa Golf Club pamoja na kutumia asilimia 29 ya siku zake za Urais kutembelea miradi yake mikubwa.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini