Mgeni rasmi Mhe. Prof Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akipokelewa kwa kwenye mahafali na kilele cha miaka 20 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyika Desemba 18, 2020.
Mgeni rasmi Mhe. Prof Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akitoa hotuba katika mahafali na kilele cha miaka 20 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyika Desemba 18, 2020.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakam ana Jaji wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Dkt. Paul Faustine Kihwelo akitoa neno la Ukaribisho katika mahafali ya ishirini na kilele cha Miaka ishirini ya Chuo.
Mgeni rasmi Mhe. Prof Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama waliotumikia chuo kwa zaidi ya miaka 10 kwenye mahafali na kilele cha miaka ishirini ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyika Desemba 18, 2020.
Wahitimu wa Stashahada ya Sheria wakiwa wanasikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
Wahitimu astashahada ya sheria wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mhe. Prof Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na viongozi wengine Katika mahafali ya 20 na kilele cha miaka ishirini ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyika Desemba 18, 2020.
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kutumia elimu waliyoipata kwa kuchambua kwa kina changamoto zilizoko kwenye jamii.
Prof. Juma alisema hayo katika sherehe za mahafali ya 20 na kilele cha miaka ishirini ya uhai wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa wahitimu wa Stashada na Astashahada ya Sheria, yaliyofanyika leo Desemba 18, 2020 chuoni wilayani Lushoto mkoani Tanga.
Katika hotuba yake iliyosheheni pongezi nyingi kwa Chuo, Jaji Mkuu amesema wakati Chuo kinaanzishwa kulikuwa na dhamira kadhaa ikiwepo kuondoa uhaba wa Mahakimu kwa mahakama za mwanzo na kuwaandaa makarani wa mahakama ili kuondoa upungufu wa kada ya makarani katika mahakama.
Aidha, Jaji Mkuu alisisitiza na kuiasa Menejimenti ya Chuo kuendeleza viwango vya kiutumishi na kimaadili ili Chuo kiendelee kuwa na sifa ya kuifanya Stashahada ya IJA kuwa ni moja ya sifa ya masomo ya ziada ya juu katika ngazi ya vyuo vikuu.
Pamoja na pongezi hizo, Jaji Mkuu aliendelea kusisitiza Uongozi wa Chuo kuwatayarisha wanafunzi wa Astashahada na Stashahada ili waendane sambamba na mabadiliko makubwa yaliyopo katika matumizi ya TEHAMA katika huduma za kimahakama nchini Tanzania ili kuondokana na mfumo wa matumizi ya makaratasi.
“Mahakama isiyojifunza au Mahakama isiyojiendeleza ni Mahakama ambayo itakabaki karne ya 19”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, Mhe. Dkt. Gerald Ndika, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, alisema kutokana na vigezo vilivyoko katika sekta ya sheria hivi sasa, miongoni mwa wahitimu wanaotoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto huajiriwa na Serikali katika nafasi za Watendaji wa Vijiji (VEO) na Watendaji wa Kata (WEO).
Dkt. Ndika aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na Chuo kukabiliwa na changamoto mbalimbali, kimeendelea kufanya vizuri katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, TEHAMAna alisema kwa kushuhudia hilo, Chuo kimeendelea kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kimataifa.
Naye Mkuu wa Chuo, Mhe Dkt.Paul Kihwelo, Jaji wa Mahakamu Kuu ya Tanzania alitoa takwimu kuwa wanachuo waliodahiliwa toka Chuo kuanzishwa ni 9,429 na kuongeza kuwa mpaka sasa Chuo kinapotimiza miaka ishirini toka kuanzishwa kwake kina jumla ya wahitimu 6,833.
Dkt. Kihwelo alishukuru Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika usajili wa 2020/2021 kwani jumla Chuo kimeletewa wanafunzi 235 waliomaliza kidato cha nne ambao majina yao yaliletwa moja kwa moja Chuoni.
Mahafali yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka idara mbalimbali za Serikali. Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi, watumishi waliotumikia Chuo toka kuanzishwa kwake na wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments