Kenya yapiga marufuku uagizaji wa magari yaliyotumika zaidi ya miaka 8 ByPascal Mwakyoma TZA | ZamotoHabari.


Habari kutoka Gazeti la Standard la Kenya zinasema kuwa idara ya viwango ya Kenya imeimarisha usimamizi wa magari ya mitumba yanayoingizwa nchini humo.


Katika taarifa iliyotolewa na idara hiyo kwa waagizaji wa magari, raia wanaorejea nchini humo na wanadiplomasia  ni marufuku kuagiza magari ya zamani yaliyotumika zaidi ya miaka 8.


Utafiti wa hivi karibuni wa African Trends and Insights umesema kuwa asilimia 85 ya magari yaliyoingizwa Kenya ni magari yaliyotumika.


Mwaka wa 2019, Serikali ya Kenya ilitoa mapendekezo mfululizo ya kuchukua hatua mpya zinazolenga kulinda wanunuzi wa magari ya ndani, na kufanya iwe ngumu na ya gharama kubwa kuagiza magari ya mitumba.


Serikali ya Kenya pia imepanga kuzuia magari ya mitumba ambayo yanatarajiwa kupunguzwa kutoka miaka minane hadi miaka mitano, na kusaidia Kenya kuimarisha usimamizi wa usalama barabarani na kupunguza uchafuzi wa hewa.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini