Lil Wayne ameweka wazi kuwa hakutakuwa na Nicki Minaj wala Drake mwingine kwenye ulimwengu wa Hip Hop. Akipiga stori na Brett Berish CEO wa Sovereign Brands juzi Ijumaa kwenye IG Live, Weezy alisema hatokuja tena kuwatoa wasanii wakafikia hatua walizofika Drake na Nicki Minaj.
-"Hakuna kitu kama hicho cha Nicki Minaj au Drake ajaye" alijibu Lil Wayne baada ya kuulizwa kama anatafuta tena warithi wa wakali hao toka Young Money. Sababu kubwa aliyoitaja ni uwepo wa mitandao ya Kijamii;
-"Huko nyuma, kipindi nawagundua Drake na Nicki Minaj muziki ulikuwa tofauti. Walitoka kipindi ambacho bado mitandao ya kijamii haijachukua nafasi. Hivyo walikuja wakati muziki ukiwa umechukua umakini wa watu. Nikimaanisha, ulimfanya kila mmoja awe nahamu ya kutaka kuona nani anafuata na kipi kinafuata kwenye muziki? Hivyo unakuwa na chaguo lako. Lakini kwa sasa hivi haiko hivyo, kuna takribani vitu vipya 1000 kwa siku." alieleza Wayne.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments