*********************************
NA DENIS MLOWE, IRINGA .
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya CCM, Rose Tweve kwa kushirikiana na kikundi Cha Sauti ya mwanamke Mafinga (MAFINGA WOMEN VOICE) wamefanikiwa kumchangia mwanamama aliyejifungua watoto wanne zaidi ya sh milioni 1 kwa ajili ya malezi ya watoto hao.
Licha ya Rose Tweve aliyechangia sh. 500,000 na kikundi hicho kutoa sh. 430,000 wengine waliochangia malezi ya watoto hao ni mbunge wa viti maalum Nancy Nyalusi aliyetoa sh. 20000 na katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda alichangia sh. 270000. Seneda licha ya kuchangia fedha hizo alitoa ahadi ya kuwafadhili maziwa watoto hao kwa muda wa miaka miwili.
Hafla hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya uwezeshaji wa akina mama katika nyanja Mbalimbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo kupinga ukatili wa kijinsia. Kupitia hafla hiyo *Mafinga Women Voice licha ya kuchangia fedha hizo kwa ajili ya mama aliyejifungua watoto wanne pia walitoa Tsh. 200,000/= kwa ajili ya vikundi viwili vya akina mama wauzaji wa matunda mjini Mafinga.
Vilevile Rose Tweve alichangia *Tsh. 1,000,000/= kwa ajili ya vikundi viwili vya akina mama vinavyo jishughulisha na uuzaji wa matunda vilivyoko mjini Mafinga.
Naye Katibu Tawala wa mkoa *Bi Happiness* alichangia *Tsh. 270,000/=* kwa ajili ya malezi ya watoto hao na kuahidi kuendelea kuwafadhili maziwa kwa muda wa miaka miwili.
Katika halfa hiyo iliyopewa jina la Mafinga women voice white party ilikuwa na kauli mbiu ya “MWANAMKE NI NGUZO KATIKA JAMII, TUMUUNGE MKONO.”
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments