Ni Kweli Wivu wa Mapenzi ndio Chanzo cha Mauaji? | ZamotoHabari.



Kufuatia kukithiri kwa matukio ya mauaji na ukatili wa aina mabalimbali  ambayo yanahusishwa na wivu wa mapenzi nchini athari za kisaikolojia zimetajwa kuwa ni moja ya sababu inayopelekea watu kufanya matukio ya ukatili.


Akizungumza katikia kipindi cha Supa Breakfast,  Mwanasaikolijia, Alexedes Kamugisha amesema kuwa mapenzi peke yake sio sababu ya moja kwa moja inayopelekea mtu kufanya matukio ya kikatili bali namna  mtu ameathirika kiundani hupelekea kufanya matukio hayo.


“Kisababishi cha watu kufanya matukio ya ukatili ni kutokana na namna wanavyoathirika kisaikolojia kutokana na tofauti zinazotengenezwa na haiba ya mtu ambapo moja wapo ni kuwa na hali ya kughadhabika, kukosa hali ya kuelewa hisia za wengine” amesema Kamugisha


Aidha kwa upande wa namna ya kusaidia kuiepusha jamii na matatizo hayo, Kamugisha ametaka malezi katika ngazi ya familia kwa watoto yapewe kipaumbele ili kuepusha matatizo ya kisaikolojia.


“Malezi yapewe kipaumbele kuhakikisha tofauti za mama na baba haziathiri watoto pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya kimwili hususani ya kihisia kwa watoto yanapatikana bila tofauti zao kuingilia" amesema Kamugisha




APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini