Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza jambo katika hotuba yake na wananchi pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo katika ngazi ya Mkoa yamefanyikia katika viwanja vya shule ya msingi majengo vilivyopo Wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ameshika na kuangalia moja ya bidhaa ambayo inazalishwa na kikundi cha wanawake wajasiriamali Wilayani Bagamoyo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya ukimwi duaniani amabyo kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Bagamoyo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dr. Delphine Magere akifafanya jambo kwa wananchi na viongozi mbali mbali wa serikali na mashirika ya umma waakti wa sherehe za maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani amabyo kimkoa yamefanyika katika shule ya msingi majengo iliyopo Wilayani Bagamoyo.
Mmoja wa wawakilishi wa baadhi ya watu wanaoishi na maambukizi ya vurusi vya ukimwi VVU Elizabeth Hassan akisoma risala kwa mgeni rasmi kuhusiana na mwenendo mzima wa baadhi ya changamato mbali mbali wanazokutana nazo na kusaidiwa na serikali.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo bada ya kupatiwa fursa ya kuzungumza na wananchi waliohudhulia katika sherehe hizo za siku ya maadhimisho ya ukimwi duniani.
Mmoja wa kijana mbaye anaishi Wilayani Bagamoyo anayejulikana kwa jina la Juma Mohamed akiwa anatoa ushuhuda kwa mgeni rasmi kuhusu madhara yanayotokana na utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo yalimsababishia kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi japo kwa sasa ameshaacha kutumia na anaendelea na matibabu.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
…………………………………………………………………………
VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameitaka jamii kuachana na tabia ya kuwabagua na kuwanyanyapaa baaadhi ya watu wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi VVU na badala yake wawape ushirikiano wa kutosha na kuwashirikisha katika shughuli mbali mbali za kuleta maendeleo pasipo kuwaonea.
Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambapo katika ngazi ya kimkoa yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi majengo Wilayani Bagamoyo na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na wadau mbali mbali wa afya kwa lengo la kuweza kutoa ujumbe walionao kuhusiana na VVU.
“Kitu kikubwa mimi kama kiongozi wetu wa Mkoa wa Pwani natambua kuwa mtu akipata maambukizi ya virusi vya ukimwi sio kwamba ndio mwisho wake wa kufanya kazi au kuendelea kuishi kikubwa akizingatia vizuri maelekezo kutoka kwa watalaamu wa afya ataweza kuishi kama watu wengine ili kubwa zaidi ninawaomba sana msiwanyanyapae kabisa kwani ni ndugu zetu na pia ni rafiki zetu tuendelee kushirikiana nao katika mambo mbali,”alisema Ndikilo
Pia katika hatua nyingine Mkuu huyo amewataka viongozi wote wa Halmashauri za Wilaya ya mji wa Kibaha, Mkuranga na Chalinze kuhakikisha kwamba wanaweka mpango mkakati kabambe ambao utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza hali ya maambukizi ya mapya ya Virusi vya ugonjwa wa Ukimwi kwani katika maeneo hayo hali sio nzuri sana kutoka na maambukizi kubwa makubwa.
Ndikilo alisema Halmashauri hizo zimeeleza kuongoza kwa maambukizi mapya ya VVU huku chanzo kikielezwq kuwa ni muingiliano wa shughuli za kiuchumi,
Alisema takwimu za maambukizi kwa Mkoa huo za mwaka 2012 ni asilimia 5.9 na kwamba kimeahuka hadi kufikia asilimia 5.5 kwa mwaka 2017.
Alisema pamoja nankushukuka kwa maambukizi lakini bado Halmashauri hizo zinaonekana kuwa na maambukizi mengi sababu sikielezwa kuwa biashara, Viwanda vingi na vituo vya magari makubwa.
Hata hivyo maambukizi kwa wanawake kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu yanaelezwa kufikia asilimia 4.3 huku wanaume wakiwa ni asilimia 3.6.
Ndikilo alisema moja ya vikwazo vinavyoelezwa kuchochea maambukizi mapya ni pamoja na mila potofu, ndoa za utotoni na ngoma za usiku.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dr. Delphine Magere aliwataka wanawake wa mkoani humo kuwa wa kwanza katika kupinga wimbi la maambukizi mapya ya VVU kutokana na umuhimu wao kwenye majukumu ya kifamilia na kuhakikisha kuwa wanaendelea kujikinga zaidi ili wasiweze kupata maambukizi mapya.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa alisema kwamba katika kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi wataendelea kushirikiana bega kwa bega na wadau wengine wa sekta ya afya pamoja na kutoa elimu mbali mbali kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuweza kwenda kupima ili kujua afya zao pamoja na kuzingatia maelekezo mbali mbali ambayo yanatolewa na watalaamu wa afya.
Awali akisoma risala ya Watu wanaoishi na VVU mmoja wa wawakilishi watu hao Elizabeth Hassan alisema kuwa kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kikwazo kilichopo katika kundi hilo ni baadhi ya Watu wanaoishi na VVU kusitisha kutumia dawa za kurefusha maisha kitu ambacho ni kinyume kabisa na maelekezo waliyoyopatiwa na madaktari.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments