ST. MARY'S KUONGEZA USHIRIKIANO NA NA SHULE ZA NJE YA NCHI, KUBORESHA MIFUMO YA KOMPYUTA | ZamotoHabari.

Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa Shule za St. Mary's, Mutta Rwakatare amesema kuwa watakuwa na Ushirikiano ya karibu kati ya Shule wanazoziongoza na shule za nje ya nchi ili kuongeza utaalamu zaidi kwa watoto wanaosoma shule hizo.

Hayo ameyasema katika Mahafali ya 22 ya shule ya St. Mary's-Mbagala yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwa watoto wanaosoma elimu ya awali. amesema kuwa watoto hao kwa wakitaka kuanza darasa la kwanza nafasi zao zipo na haiitaji kufanya usajili tena.

Amesema kuwa watakuwa wanabadilishana wanafunzi pamoja na walimu kutoka nchi tofauti kwa kwenda na kurudi.

"Huu ni mpango Mkakati wa Shule zetu zote ikiwa ni kwaajili ya kuboresha taaluma za shule zote za St. Mary's zilizopo Dar Es Salaam- Mbagala, Tabata, Mbezi, Dodoma, Ifakara, Mbeya na Morogoro." Amesema Rwakatare

Hata hivyo amesema kuwa wanampango wa kuboresha madarasa yatakayokuwa yanatoa elimu ya Tehama na mifumo ya Kompyuta kwa wanafunzi (Computer Clases) ili kuhakikisha watoto kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la saba wapate ujuzi wa kutumia kompyuta kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia kwa karne ya sasa.

Rwakatare pia amesema wataweka mkazo katika michezo ili kuwasaidia wanafunzi ambao watakuwa na vipaji mbalimbali katika michezo kwa kuwapa walimu ambao wanafundisha michezo ile ili kukuza vipaji vyao.

Hata hivyo amewaomba ambao hawajawapeleka watoto wao katika shule za St. Marry's kuwapeleka ili wakapate malezi bora na yenye tija kwa jamii kwa maboresho yanaendelea katika shule zote.

"Kuna maboresho makubwa ambayo tumeyaboresha katika shule zetu, miundo mbinu, mabweni, madarasa pamoja na mifumo ya Kompyuta ili kuhakikisha watoto wanaishi vizuri wawapo shuleni na kupata elimu iliyo bora." Amesema Rwakatare.

Hata hivyo katika mahafali hayo watoto waliweza kuonesha vipaji vyao katika kuimba, kuelezea mfumo wa chakula pamoja na kuonyesha mitindo mbalimbali ya mavazi huku wakionesha ustadi katika miondoko ya mitindo hiyo.
Viongozi mbalimbali wa shule ya Kimataifa ya St. Mary's wakiwa katika picha ya pamoja na watoto waliohitimu masomo kwa ngazi ya awali katika mahafali ya 22 shule hiyo yaliyofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakitumbuiza huku wakiwa na mavazi ya Mitindo ya kawaida katika mahafali ya 22 ya shule ya Kimataifa ya St. Mary's iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakinesha vyeti vyao aada ya kutunukiwa katika mahafali ya 22 ya shule hiyo.
Burudani ikiendelea.

Wazazi wakipata burudaani katika mahafali ya 22 ya wanafunzi wa ngazi ya awali wanapohitimu masomo yao na kuanza Darasa la kwanza.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini