Video Vixen na mpenzi wa msanii Whozu, Cappuccino Tunda amesema moja ya tabia yake akiwa amelewa huwa anapenda atamfuata mpenzi wake popote alipo hata kama atakuwa ameleweshwa na watu wengine.
Cappuccino Tunda ameeleza hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo ameandika kuwa "Pisi yako ikilewa inapenda kufanya nini, mimi nikilewa lazima nimfuate 'boyfriend' wangu alipo hata kama nimeleweshwa na watu wengine, simu moja tu sipo"
Mahusiano ya Tunda na Whozu yalianza muda mrefu tangu wakiwa shuleni wanasoma huko Moshi, Kilimanjaro ila waliachana kisha kurudiana tena mwaka 2018.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments