Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akihutubia Wadau wa Mkutano wa Kikanda wa Uwekezaji na Biashara ya Mazao ya Bustani katika ukumbi wa Hoteli ya Hayatt Regency ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akihutubia Wadau wa Mkutano huo wa Kikanda wa Uwekezaji na Biashara ya Mazao ya Bustani ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Abubakar Kunenge.
Mtendaji Mkuu wa Asasi ya Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt. Jacqueline Mkindi akihutubia Wadau wa Mkutano huo wa Kikanda wa Uwekezaji na Biashara ya Mazao ya Bustani ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Abubakari Kunenge, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Asasi ya TAHA pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya wakimuaga Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani amara baada ya kufungua Kongano la Kikanda la Uwekezaji na Bustani ya Mazao ya Bustani,
………………………………………………………………………………………………
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya amemuahidi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na Wadau wa Sekta ya Kilimo cha mazao ya bustani kuwa Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana na Wizara nyingine kama Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Balozi za Tanzania nje ya nchi katika kutafuta masoko ya mazao ya bustani (Mbogamboga, matunda, maua na viungo) ili kuongeza akiba ya fedha za kigeni nchini.
Katibu Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya ameyasema hayo wakati akiwahutubia Wadau wa Mkutano wa Kikanda wa Mazao ya bustani; Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Hayatt Regency ambapo Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Asasi ya Mazao ya Bustani (TAHA) zilianda mkutano huo wa siku moja.
Katibu Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya ameongeza kuwa mwaka 2019 Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilifanya utafiti wa masoko katika nchi za Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Nchi za Kiarabu ambapo kupitia Ushirikiano huo, Tanzania iliuza mazao kwenye nchi hizo.
Pamoja na mazao ya bustani kuuzwa katika nchi ya Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Farme za Kiarabu; Jumla ya dola milioni 779 za Marekani zilipatikana kutokana na uuzwaji kuuza mazao hayo duniani kote.
“Tayari, zaidi ya tani 150 za parachichi, mananasi na pilipili kali zimekwishauzwa kwenye hayo masoko jambo ambalo ni matokeo makubwa ya namna ambavyo Serikali inaweza kufanya kazi na sekta binafsi na kuleta matokeo makubwa chanya.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
Katibu Mkuu Kusaya ameongeza kuwa suala la kutafuta masoko ya uhakika ni mkakati wa kitaifa.
“Ili kuweza kuyafanyia kazi kwa mapana yake masuala ya upatikanaji wa masoko, Wadau wa Sekta ya Kilimo, kupitia Kamati ya Ufundi yenye wawakilishi toka taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi imeanza kuandaa Mkakati wa Masoko ya mazao ya bustani au kwa kiingereza Horticulture Industry Market Access Strategy – HIMAS). Mkakati huo utaainisha maeneo muhimu ya kufanyiwa kazi ili kuboresha upatikanaji wa masoko na kutukwamua toka hapa tulipo.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
Katibu Kusaya ameongeza kuwa ili kuimaisha usimamizi wa masuala ya afya ya mimea na viuatilifu, mwezi Juni mwaka 2020 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria mpya ya Afya ya Mimea ambayo pamoja na mambo mengine inaanzisha Mamlaka ya Afya ya Mimea na Udhibiti wa Viuatilifu na kuongeza kuwa hatua hiyo imelenga kuimarisha usimamizi na huduma kwa kuwa na Mamlaka moja itakayosimamia shughuli zilizokuwa zilizokuwa zinafanywa na TPRI na Kitengo cha Afya ya Mimea cha Wizara ya Kilimo; Ambapo kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo kutaongeza ubora wa mazao yakiwemo, mazao ya horticulture kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.
Kwa kuongezea Katibu Mkuu Kusaya amesema Wizara ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana na Wadau kuzipatia ufumbuzi changamoto katika Sekta ya kilimo ili Sekta iendelee kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi, ajira na upatikanaji wa malighafi za viwanda ambapo takribani asilimia 5 za makighafi za viwanda zinategemea kilimo.
Aidha Katibu Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya ameipongeza Asasi ya TAHA inayoongozwa Dkt. Jacqueline Mkindi kwa kufanikisha mkutano huo na kuongeza kuwa Yeye kama Mtendaji Mkuu ataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa tasnia ya mazao ya bustani inasonga mbele.
“Niseme kwamba jitihada hizi za Wizara kwa kushikiana na Sekta Binafsi chini ya uratibu wa TAHA; Zote zinalenga kuifanya nchi yetu kuwa mhimili wa uzalishaji na usambazaji wa mazao ya horticulture na mazao mengine kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Masoko ya Kikanda, yanaonekana kuwa fursa kubwa kwa kilimo chetu cha mazao ya bustani (horticulture) na leo hii tunakutana ili kutafuta namna ambavyo nchi yetu inaweza kufaidika nayo. Wizara ya kilimo itaendelea kuratibu shughuli za kuimarisha Sekta hii na kuhakikisha kuwa Wakulima wanafaidika nayo.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments