Kitunguu swaumu pamoja kuwa ni dawa ambazo humsaidia mwanadamu kuweza kutibu magonjwa mbalimbali lakini kinatajwa kuweza kutibu magonjwa mbalimbali ya wanyama wengine ikiwemo kuku.
Zipo dawa tofauti za asili zinazopatikana kirahisi kwenye mazingira ya vijijini na mjini ambazo zina uwezo wa kutibu magonjwa ya kuku. Katika mada hii tataelezea jinsi kitunguu swaumu kinavyoweza ugonjwa wa Homa ya Matumbo "Fowl Typhoid" katika ufugaji wa kuku.
Namna ya kuandaa dawa hii.
Chukua robo kilo ya vitunguu swaumu
Toa maganda.
Kisha twanga
Changanya na maji kiasi cha lita moja
Chuja na kuwapa maji yake kuku wako kwa muda wa juma moja.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments