Utafiti mpya uliotolewa leo unaonesha idadi kubwa ya watu duniani haitaweza kupata chanjo ya Covid-19 hadi 2022, huku kwa mataifa tajiri kukiwa na uwezekano wa zaidi ya nusu kuipata katika nusu ya mwanzo ya 2021.
Katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na matumaini kwamba chanjo hiyo inaweza kuzuia janga hilo ambalo limesababisha vifo vya takribani watu milioni 1.6, mataifa kama Marekani, Uingereza na Umoja wa Falme za Kiarabu yameanza programu za utoaji wa chanjo wa kwa watu wake. Na bado yapo katika jitihada ya kutanua zaidi huduma hiyo katika maeneo tofauti ya mataifa yao.
Utafiti wa asasi yenye kujikita katika masuala ya afya ya John Hopkins Bloomberg unaonesha mataifa tajairi ambayo yanafanya jumla ya asilimia 14 ya idadi wote duniani yameagiza zaidi ya nusu ya dozi ya chanjo ambayo itarajaiwa kuzalishwa na makampuni 13 hadi mwaka ujao.
Kumekuwepo na mashaka kwamba mataifa masikini yataachwa nyuma. Lakini hata kama watengenezaji wa dawa wote watatoa chanjo bora, salama na kufikia malengo yao ya kiwango cha juu cha utengenezaji, utafiti huo mpya unasema "bado idadi kubwa ya watu ulimwenguni hawatapata chanjo hadi 2022".
Utafiti huo, ambao umechapishwa katika jarida la kitabibu la BMJ unaonesha hadi katikati ya mwezi uliopita wa Novemba kulikuwa na hifadhi ya dozi bilioni 7.48, kiwango ambacho unaweza na kukilinganisha na mtiririko wa utoaji chanjo milinoni 3.76, kwa sababu kwa kawaida, sehemu kubwa ya chanjo inapaswa kufanyika mara mbili. Kwa hivyo kwa makadirio hayo upo uwezekano wa kutabiri uzalishwaji wa dozi bilioni 5.96 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2021.
Asilimia 40 ya chanjo inaweza kuyafikia mataifa yenye kipato duni
Utafiti huu mpya unakadiria pia hadi asilimia 40 ya chanjo kutoka kwa makampuni yanayoongoza kwa uzalishaji,inaweza kupatikana kwa mataifa yenye kipato kidogo na cha kati, lakini hata hivyo ulisema hatua hiyo itategemea mataifa matajari yatakavyewza kugawa kile ambacho imekinunua. Watafiti wamehimiza kile walichokiita "uwazi zaidi na uwajibikaji" katika kuunga mkono usawa wa kuufikia ulimwengu
Mataifa mengi yamejiunga katika chombo cha ununuzi kinachoratibiwa na Shirika la Afya la Ulimwenguni WHO, Umoja wa Uvumbizi wa Kujihami na Majanga na Muunganao wa Chanjo ujulikanao kama GVI, kwa lengo la kuhakikisha watu wote wanapata chanjo ya COVID-19 katika maeneo tofauti ya ulimwengu pasipo kujali uwezo walionao, lakini jitihada hiyo inaweza kufanikisha upatikanaji dozi bilioni mbili tu, hadi mwishoni mwa mwaka 2021. Lakini pia sio Marekani wala Urusi ambazo zimejiunga na mpango huo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments