Zaidi ya watu milioni 16 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani. Hii ni kulingana na hesabu ya chuo kikuu cha John Hopkins hapa Marekani. Zaidi ya watu 307,000 wamefariki. Hesabu hiyo imetolewa wakati chanjo dhidi ya Corona inaendelea kutolewa kote nchini. Chanjo hiyo imeleta matumaini ya kushinda nguvu maambukizi ya Corona japo idadi ya watu wanaolazwa hospitalini inaendelea kuongezeka kwa kasi. Maafisa wanaosimamia shughuli ya kutoa chanjo hiyo wamesema kwamba wanatarajia watu milioni 20 kupata dozi za kwanza mbili zinazohitajika kabla ya mwisho wa mwaka. Wafanyakazi wa afya walio katika msitari wa mbele kupambana na janga la Corona na wahudumu katika vituo vya kuwasaidia watu wazee, ndio watu wa kwanza kupewa chanjo hiyo. Kwa wastan, watu 211,000 wanaambukizwa virusi vya Corona kila siku. Zaidi ya watu 112,000 wanalazwa hospitalini.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments