“Kufa tutakufa tu, unaweza ukafa kwa Malaria, Kansa na Magonjwa mengine, kufa kupo, ila kamwe tusimuache Mungu, Waislamu walitangaza muda wao wa kuomba, Waislamu wameanza leo, kesho Wasabato, Jumapili Wakristo kwa siku 3 kwa kuomba na kufunga tutashinda”-JPM
“Magonjwa yapo tu, Mungu hashindwi, tulishinda Mwaka jana, inawezekana hili ni jaribu jingine, tusimame na Mungu tutashinda, inawezekana kuna mahali tulimkosea Mungu, tusitishane na kuogopeshana tutashindwa kufika” -JPM
“Leo nimetumiwa meseji na Waziri wa Fedha Dr.Mpango ambaye amelazwa Dodoma, na ninaoomba niisome hapa kwa faida ya waliokuwa wanatweet kwamba amekufa, anasema ‘Rais ninakula, nafanya mazoezi na kutembea, wanaonizushia kifo mitandaoni niliwaombea msamaha kwa Yesu’, amewaombea”-JPM
“Balozi Kijazi ametangulia zamu yetu sisi bado, Watanzania katika matatizo yoyote yanapotokea yatufanye tuwe wamoja, hofu ni mbaya, ukiona kitu hauwezi kukitatua wewe, mwambie Mungu ndiye muweza, tumekuwa tunatishana sana”-JPM
“Mwaka 2000 nilipoteuliwa kuwa Waziri nikaenda Ikulu nikamuomba Mzee Mkapa, kwamba huyu Mkurugenzi wa Barabara (Kijazi) awe K/Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mzee Mkapa aliniangalia nafikiri alinishangaa, hakunipa jibu, baadaye Kijazi akateuliwa kuwa K/Mkuu alifanya kazi kubwa” -JPM
“Nilipoona kazi nzuri ya Kijazi kwa Barabara za Dodoma nikamshauri Waziri wangu Mama Anna Abdallah kuwa tumpandishe cheo ndipo Injinia Kijazi akateuliwa kuja DSM na kushughulikia Barabara zote zinazohitaji ukarabati TZ na Barabara zikawa zinapitika” -JPM
“Balozi Kijazi nina historia nae ndefu kidogo,nilipoteuliwa na Mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi mwaka 1995, nilitembelea Barabara za Dodoma nikakuta zote zinapitika, nikamuuliza Kijazi kwanini zako ni nzuri kuliko za wengine, akaniambia pesa zote anazopewa zinatumika vizuri”-JPM
“Hata baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2020, Maalim Seif alikubali maridhiano, na alikuja Chato na Rais Mwinyi, mazungumzo yake yalikuwa ya raha sana, Maalim alikuwa mcheshi, alikuwa akihubiri umoja wa Wazanzibar na Watanzania, Mungu ampokee mahali pema peponi” -JPM
“Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Maalim Seif aliniandikia barua mara tatu tofauti, baadaye nikaona nionane nae alipokuja akaniambia sijashiriki kwenye Uchaguzi ila sitohamasisha vurugu, Zanzibar itakuwa kwenye Amani,na nilithibitisha hilo kwa vitendo”-JPM
“Natoa pole kwa Watanzania wote kwa vifo vyote viwili, cha Maalim Seif pamoja na cha Balozi Kijazi, Jana nilimtuma Makamu wa Rais na Dkt. Bashiru waniwakilishe kwenye mazishi ya Maalim Seif”-JPM kwenye shughuli za kumuaga Kijazi
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments