Jacob Zuma Kikaangoni, Jaji Ataka Afungwe Gerezani Kwa Kushindwa Kufika Mahakamani Kujibu Tuhuma za Ufisadi | ZamotoHabari.

 


Jaji mmoja nchini Afrika Kusini amesema anataka aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kuhukumiwa kifungo gerezani kwa kushindwa kufika mahakamani kujibu madai ya ufisadi.

Bwana Zuma, 79, alidharau ombi la kufika mbele ya tume ya uchunguzi ambayo mwenyekiti wake ni hakimu Ray Zondo.


Jaji amesema ukaidi wa Bwana Zuma kunaweza kusababisha kutotekelezwa kwa sheria na kwamba ataomba mahakama ya juu ya Afrika Kusini kumhukumu aliyekuwa rais kwa kosa la kukiuka masharti ya mahakama.


Bwana Zuma amesema anaamini kwamba jaji Zondo alikuwa na upendeleo katika uamuzi alioutoa dhidi yake.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Awali, alikuwa ametaka jaji huyo kujiuzulu kama mwenyekiti wa jopo la uchunguzi wa kesi dhidi yake.


Jaji Zondo alitupilia mbali ombi hilo na kusema anafanya kazi yake bila upendeleo.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini