Ri Sol-ju, mke wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya muda wa zaidi ya mwaka mmoja.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya serikali, Ri Sol-ju, ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, alihudhuria tamasha la kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa baba ya mumewe na rais wa zamani Kim Jong-il.
Siku ya kuzaliwa ya Kim Jong-il ambaye ni kiongozi wa pili wa nasaba hiyo, ilianza kusherehekewa kama "Shining Star Day" na ikawa moja ya likizo muhimu zaidi nchini.
Kulikuwa na uvumi kwamba kutokuonekana kwa Ri Sol-ju kwa muda mrefu kulihusishwa na janga la corona au ujauzito.
Shirika rasmi la KCNA liliripoti,
"Kila mtu aliyehudhuria alikuwa amejawa na furaha wakati Katibu Mkuu alipoingia kwenye ukumbi wa michezo na mkewe Ri Sol-ju kwa muziki wa mapokezi."
Katika picha iliyochapishwa na wakala, ilionekana kuwa hakuna mtu yeyote kati ya waliohudhuria aliyevaa barakoa.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments