NITAENDELEA KUWA KARIBU NA WATANZANIA- KOFFI OLOMIDE | ZamotoHabari

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na mwanamuziki galacha duniani katika muziki wa rhumba, Koffi Olomide aka Mzee ya Mboka, walipokutana usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam ambapo mwanamuziki huyo alikuwa nchini kutumbuiza chini ya mwaliko wa kampuni ya Prime Time Promotions na Clouds Intertainment.

Dkt. Abbasi alitumia muda huo kumshukuru mkongwe huyo kwa kuitangaza Tanzania mara kwa mara ikiwemo kushirikiana na wanamuziki vijana wa hapa nchini kuinua na kuutangaza muziki wao. Koffi aliahidi kuendelea kusaidia kukuza vipaji vya Tanzania akisema: "Dar es Salaam na Tanzania mimi ni kama nyumbani, nitaendelea kuwa nanyi karibu."

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha mbalimbali na Mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyekuwa akitumbuiza katika tamasha la Mahaba ya Rhumba Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi  akimsikiliza  Mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyekuwa akitumbuiza katika tamasha la Mahaba ya Rhumba Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi  akimueleza jambo  Mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyekuwa akitumbuiza katika tamasha la Mahaba ya Rhumba Jijini Dar es Salaam.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini