Na John Nditi, Morogoro
WAZIRI wa Kilimo Profesa, Adof Mkenda amesema ifikapo mwaka 2022 Serikali haitoa vibali vya kuagiza sukari nje kwa makampuni ya uzalishaji sukari .
Kwa sasa kampuni hizo zimetakiwa kuongeza uchakataji wa miwa ya wakulima inayolimwa na kushindwa kuvunwa kila mwaka ili kuwezesha kuzalisha sukari ya kutosha mahitaji ya ndani.
Profesa Mkenda alitoa kauli Februari 15, mwaka huu (2021) kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na uongozi wa mkoa wa Morogoro pamoja na uongozi wa kiwanda cha Sukari cha Kilombero akiwa ziarani kukagua hali ya uzalishaji sukari na kuongea na wakulima wa miwa.
Waziri wa Kilimo ,alisema kwa sasa serikali inafuatilia kwa karibu utendaji kazi wa viwanda vya kuchakata sukari nchini.
Pamaoja na hayp pia alimwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kupatia mikataba ya viwanda vya sukari ili kuona kwa nini haioneshi utashi kkuongeza uwingo wa viwanda ili viweze kuchakata miwa yote ya wakulima.
-
"Nisema wazi kuwa shida yetu ya sukari haitokani na kukosa miwa bali ni uwezo mdogo wa viwanda kuchakata miwa yote ya wakulima nchini hali inayosababisha baadhi ya miwa ya wakulima kukosa soko na kuharibikia mashambani " alisema Profesa Mkenda.
Waziri wa Kilimo alisema ; “ Tunapenda wakulima wawe wanalima miwa yao na inatumika yote katika viwanda ili serikali iweze kujitosheleza kwa sukari na kupunguza uingizaji wa ndani “ alisema Profesa Mkenda.
Hata hivyo alisema , kwa miaka mitano ya awamu ya kwanza ya Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli imeondoa vitendo vilivyosababisha wazalishaji wa ndani wa sukari kushindwa kumudu ushindani wa soko kutokana kuingizwa sukari nyingi kutoka nje.
“ Kwa sasa mazingira ya tasnia ya sukari ni mazuri na hata imefikia uingizaji wa sukari kutoka nje kuwa wastani wa tani 40,000 ili kufidia upungufu , sasa tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye viwanda vya kuchakata miwa ya wakulima inayolimwa kwa wingi” alisema Profesa Mkenda.
Kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Sukari Tanzania uzalishaji kwa mwaka ni takribani tani 300,000 ambapo kwa mwaka 2020/21 ulifikia tani 377,527 na mahitaji ya sukari kwa matumizi ya kawaida na viwandani ni tani 655,000 .
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalobelo, alimkaribisha waziri, alisema kwenye tasnia ya sukari mkoa una viwanda vitatu ambavyo ni Kilombero 1 , Kilombero 11 pamoja na Kiwanda cha Sukari Mtibwa.Hata hiyo , alisema kwa sasa kuna mchakato unaendelea kufanyika kwa ajili ya kuwezesha kuwanzishwa viwanda vingine viwili vya Sukari.
Waziri wa Kilimo Profesa, Adof Mkenda akifafanua jambo wakati akizungumza na uongozi wa serikali ya mkoa wa Morogoro ukiongozwa na Katibu Tawala wa mkoa huo , Mhandisi Emmanuel Kalobelo pamoja na watendaji wa tasnia ya Sukari nchini akiwa kwenye ziara ya kukagua hali ya uzalishaji sukari na kuongea na wakulima wa miwa na ( kushoto) ni katibu mkuu wa wizara hiyo, Gerald Kusaya.
Waziri wa Kilimo Profesa, Adof Mkenda akieleza jambo wakati akizungumza na uongozi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero pamoja na viongozi wa tasnia ya Sukari kutoka Taasisi zilizopo chini ya wizara yake akiwa kwenye ziara ya kukagua hali ya uzalishaji sukari na kuongea na wakulima wa miwa,
Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro , Mhandisi Emmanuel Kalobelo akitoa taarifa ya hali ya sekta ya Kilimo kwa Waziri wa Kilimo Profesa, Adof Mkenda , akiwa kwenye ziara ya kukagua hali ya uzalishaji sukari na kuongea na wakulima wa miwa..
Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Sukari Kilombero (KSCL), Balozi Ami Mpungwe akielezea hali ya uzalishaji wa sukari katika viwanda vya Kilombero kwa Waziri wa Kilimo Profesa, Adof Mkenda, kwenye ziara ya kukagua hali ya uzalishaji sukari na kuongea na wakulima wa miwa.( Picha zote na John Nditi).
Wadau kutoka taasisi za tasnia ya sukari
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments