Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAJUMBE wa Baraza la wadhamini la Chama Cha Mapinduzi ,(CCM) limewataka viongozi wa vyama vya upinzani nchini kujiunga na Chuo cha uongozi na Itikadi cha Mwalimu Nyerere ,kilichopo Kwamfipa,Kibaha,mkoani Pwani, ili kujiongezea uwezo na kujifunza maadili na uzalendo wa nchi yao.
Walizungumza hayo mara baada ya kukagua majengo ya chuo hicho,wakati walipofanya ziara ya kutembelea chuo hicho ,kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa chuo hicho.
Mwenyekiti wa baraza hilo ,ANNA ABDALLAH na makamu wake PANDU OMARY KIFICHO walisema, vyama imara kama CCM viongozi wake huandaliwa kuwa na maadili na uzalendo hivyo hivyo chama chochote kinachotaka kujiimarisha basi kipeleke viongozi na vijana wao kupikwa katika chuo hicho .
Hata hivyo ,walielezea, baraza limeridhishwa na kukamilika kwa ujenzi huo ambapo hatua iliyoko sasa ni kukamilisha kupitisha rasimu ya mitaala.
Anna alishauri kuingiza somo uzalendo na maadili kwa wanafunzi watakaopikwa katika chuo hicho hususani vijana waweze kujua historia ya nchi yao
PANDU OMARY KIFICHO ambae ni Makamu mwenyekiti wa baraza hilo ,aliwataka vijana kujiunga na Chuo hicho ili kupata mafunzo yatakayowapa maarifa watakapofanikiwa kuwa viongozi kwenye ngazi mbalimbali.
Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogoro alisema kuwa wataendeleza fikra za hayati Mwalimu Julius Nyerere.
"" Ambapo na ujenzi wa Chuo hiki unatekeleza kwa vitendo fikra hizo na wanavyowaona viongozi waliotangulia wanapata faraja"aliongeza Mpogolo.
Msimamizi wa mradi huo, EMANUELA KAGANDA ,alifafanua, mradi huo umekamilika kwa upande wa Ujenzi wa majengo ,umegharimu kiasi cha sh.bilioni 90, na kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 200.
Alisema kuwa, ujenzi huo ulianza mwaka 2018, ambapo amedai umechelewa kutokana na hali ya mvua pamoja na kuibuka kwa ugonjwa wa Covid-19 Corona.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments