Kajala Masanja Arudisha Mali za Harmonize | ZamotoHabari.



UKIMZINGUA anakuzingua kwelikweli! Huyo ndiye Kajala Masanja, staa wa Bongo Muvi ambaye anadaiwa kumrudishia vitu vyote staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ambavyo alimpa wakati wakiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi, RISASI linapa mchapo kamili.


Kajala anadaiwa kufanya hivyo ikiwa ni kuonyesha hahitaji chochote cha msanii huyo kibaki maishani mwake kutokana na jinsi alivyomzingua.

TUJIUNGE NA CHANZO

Akizungumza mtoa habari wetu makani ameeleza kuwa, baada ya kutokea ugomvi kati ya wapendanao hao, Kajala ameamua kurejesha kila kitu ikiwemo gari aina ya Toyota Crown, alilokuwa amepewa na mpenzi wake huyo kabla ya kumwagana.


“Jamani Kajala amerudisha kila kitu nasikia hata lile gari alilompa Harmo na vitu vingi ambavyo alimpa wakiwa kwenye uhusiano mzuri ambao ulibamba kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii,” kilisema chanzo.

ANATEMBELE NINI?


Chanzo hicho kilipoulizwa Kajala kwa sasa atakuwa anatumia usafiri gani, kilisema suala la usafiri kwa Kajala sio ishu kwani pesa anayo na muda wowote anaweza kununua gari lake.“Kajala pesa ipo na hajawahi kukaa muda mrefu bila kuwa na gari labda mwenyewe tu aamue kuuza lakini magari sio tatizo kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, kwa sasa Kajala anatumia usafiri wa kukodi katika mizunguko yake ya mjini maana hata hivyo yeye mwenyewe sio mpenzi sana wa kuendesha gari.“Kajala anapenda kuendeshwa jamani, hapendi sana kuendesha yeye mwenyewe ndio maana huwa anakuwa mzito sana kununua magari,” kilisema chanzo hicho.

ASUSIA NYUMBA

Baby and dog always sleep in one room - Then her mother saw something incredible on the baby camera!
Love What Matters
by TaboolaSponsored Links
Mtoa habari wetu huyo alisema kuwa, mbali na gari na vitu vingine, Kajala pia amesusia nyumba ambazo zipo Kigamboni za Hamidu City, alizotaka Harmonize kukamilisha malipo yake kwa ajili ya Kajala na mtoto wake kwa kuwa anaamini kuwa hakuwa na mapenzi ya kweli kwao.

“Hivi unajua Kajala hata zile nyumba zinazodaiwa kuwa Harmonize alitaka kukamilisha malipo yake Kigamboni amezikataa kabisa na hahitaji tena kwani aliona kama hakuwa na nia nzuri na kila alichonunua kwake kilikuwa hakina maana halisi,” alisema mpashaji huyo.


RISASI LAMSAKA


Gazeti hili lilimtafuta Kajala kwa njia ya simu ambapo alipopatikana, aliomba na kusema kuwa hawezi kuzungumza lolote linalohusiana na msanii huyo wa Bongo Fleva.“Mimi ningeomba mniache kwanza kabisa sitaki kuzungumza chochote kuhusiana na huyo mtu nawaomba sana,” alisema Kajala.

TUMEFIKAJE HAPA?

Penzi la Kajala lililipuka ghafla mapema mwaka huu na kuwa na matuko mengi sana kwenye ulimwengu wa burudani kufuatia wao wenyewe kuyatengeneza.Walikwenda visiwani Zanzibar wakati wa Sikukuu ya Valentine Day, wakafuatiliwa sana kabla ya kitumbua chao kutiwa mchanga na Rayvanny ambaye alivujisha picha zisizo na maadili zilizomuonesha yeye akiwa na mtoto wa Kajala, Paula.


Baada ya kumaliza kimyakimya sakata hilo, ghafla hivi karibuni ndipo zilipoibuka taarifa kuwa wawili hao wamemwagana baada ya Harmonize kudaiwa kumtaka Paula na kumtumia picha chafu.

Wakati wambeya wakiwa wanatafakari hayo, Kajala akafuta picha zote alizopiga na Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram kuashiria kwamba biashara kati yao imeisha rasmi!Baada ya jambo hilo kutokea, Kajala alionekana akiwa na mwanaye Paula jijini Arusha ‘akiinjoi’ maisha huku Harmonize ambaye yeye hajafuta picha za Kajala kwenye ukurasa wake wa Instagram akiendelea na ratiba zake jijini Dar es Salaam.Inaelezwa pia, Harmonize amefurushwa kwenye nyumba ya Kajala alipokuwa anaishi na sasa haijulikani anaishi wapi.

GPL



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini