RC KUNENGE ATOA ONYO KWA WATENDAJI WA BODI YA MAGHALA NA WAKALA WA VIPIMO | ZamotoHabari.

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

MKUU wa Mkoa wa Pwani,Aboubakar Kunenge,, ametoa onyo  kwa watendaji wa Bodi ya Maghala na Wakala wa Vipimo ,mkoani humo, kushindwa kupima mizani zilizopo kwenye maghala ya vyama vya Msingi zinazotumika kupokelea Ufuta na  kushindwa kusimamia maandalizi ya Maghala Makuu, hali inayosababisha kero na kusuasua kwa zao hilo.

Alitoa onyo hilo,wakati akiendesha Mkutano wa Wadau wa Ufuta,Ikwiriri Wilayani Rufiji.

Kunenge alikerwa na watendaji hao wa Serikali kusubiri kuitwa na  Wakulima badala ya kuwafuata na kutoa huduma. 

Alieleza ,hahitaji kuona ubabaishaji,kwani hatosita kuwaondoa kwa kushindwa kusimamia wajibu wao kikamilifu.

Aidha Kunenge alitoa muda wa Siku tatu kwa watendaji hao ,kuhakisha kuwa wanakamilisha maandalizi ya Maghala  Makuu na Upimaji wa Mizani kwenye maghala ya Msingi.

 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini