AWESO ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI MANYARA | ZamotoHabari.



WAZIRI Wa Maji Mh Juma Aweso Amefanya Ziara Katika Mkoa wa Manyara hususani Jimbo La Babati Vijijini  kukagua Miradi Ya Maji Maeneo Mbalimbali Kama Ifuatavyo:

Mh Waziri amekagua Mradi Mkubwa wa Maji Minjingu Na Kuridhishwa na Maendeleo ya Mradi Huo ambao umefika 95% na kutoa maelekezo ya kwamba ifikapo tar. thelathini mwezi wa sita wakabidhi kazi hii.

Pia Mh Aweso Amekagua Mradi wa Maji Darakuta, Magugu Yote imefikia 75%,Mh Waziri amerizishwa na mwenendo wa Mradi Huo na kuwaagiza Wakandarasi kuongeza speed Ili wananchi wapate Huduma.

Waziri Aweso ambaye ameongozana na Mbunge wa Jimbo Mh Daniel Sillo, Pia wamezindua Mradi wa Maji uliokamilika Wa Endakiso na Sasa Wananchi wameanza kupata Maji.

Aidha, Aweso amewapongeza Meneja wa RUWASA mkoa wa Manyara pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Babati (BAWASA) kwa kazi nzuri na kuahidi kuwapa zawadi kama sehemu ya kutambua jitihada zao na mageuzi waliofanya Manyara.
#mageuzisektayamaji

 

 



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini