'GO NA NMB' ILIVYOZINDULIWA VIWANJA VYA TCC, CHANG'OMBE DAR | ZamotoHabari.

Naibu Waziri wa Nchi (OWM) Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi (wa tatu kulia) akipongezana na Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto) mara baada ya uzinduzi wa jukwaa la la vijana la "Go na NMB" lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya TCC, Chang'ombe wilayani Temeke, Dar es salaam. Katambi aliipongeza Benki ya NMB kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazowakabili vijana, hasa zile za masuala ya kifedha na uchumi kwa ujumla . Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe (wa pili kulia), Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Benedict Baragomwa (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Masoko Benki ya NMB, Rahma Mwapachu (kulia) pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaan, Donatus Richard. Naibu Waziri wa Nchi (OWM) Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi akizungumza katika uzinduzi huo, ambapo alisema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwamo Benki ya NMB imekuwa ikianzisha fursa mbalimbali ambazo lengo lake kuu ni kuinua vijana, lakini moja ya changamoto wanayokumbana nayo vijana ni wenyewe kutokuwa wepesi katika kuchangamkia fursa hizo hali inayofanya malengo ya serikali Pamoja na wadau wake kama NMB kutofikiwa kwa wakati na hivyo vijana wakijikuta wakiendelea kulalamika juu ya tatizo la ajira, huku tatizo likiwa wengi wa vijana hao, kutoangalia nje ya box katika kuchangamkia fursa hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe akizungumza katika uzinduzi wa Go na NMB uliofanyika jijini Dar es Salaam.






Afisa Mkuu Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi aliesema benki ya NMB imefanya utafiti wa kina kujua changamoto zinazowakabili vijana hapa nchini, na kuamua kuja na wazo la kuanzisaha jukwaa la Go na NMB, jukwaa ambalo linalenga kujenga mazingira Rafiki kwa vijan katika benki ya NMB kwa kuwahudumia Kwenye Mahitaji yao ya kibenki na kifedha.


Hivyo basi benki ya NMB inaamini kua kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni suluhisho kubwa la changaomoto zinazowakabili vijana kwenye masuala ya kifedha na uchumi kwa ujumla wake Amesema.


“Jukwaa hilo la Go na NMB litaunganisha vijana wa Nyanja zote wakiwamo wanafunzi, wakulima na wafanyabiashara, ambapo kupitia jukwaa hilo watakuwa na uwezo wa kukopa, kupata elimu ya fedha na namna sahihi ya kutumia technolojia katika kuwaletea maendeleo ya kiuchmi”. Amesema hayo katika uzinduzi huo wa Go na NMB uliofanyika jijini Dar es Salaam.











APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini