Mashabiki wa Diamond na Burnaboy wamekuwa wakitaka wapewe ‘link’ ili Wawapigie Kura Wasanii hao kuwawezesha kushinda Tuzo ya BET katika Kipengele cha Best International Act 2021.
Ukweli ni kwamba, BET hawana mfumo wa mashabiki kupiga kura (popular votes) ili kumpata mshindi, bali kura zinapigwa na akademi yao (BET Awards Voting Academy) yenye watu 500 ambayo tayari wanakuwa wamewachagua wenyewe.
Akademi hii inajumuisha watu mbalimbali wenye uelewa kutoka kwenye muziki, media, bloga, burudani na hata mashabiki ambao hupita katika mchakato maalum kabla ya kutambulika.
BET kupitia tovuti yao hutoa taarifa kuwa wanahitaji wanachama wa kupiga kura kisha wanaambatanisha na fomu ya maswali ambayo anayehitaji kuingia katika hiyo akademi atayajibu.
Maswali yanalenga kupima uelewa wa mwombaji kuhusu burudani na wale watakaojibu vizuri ndio wanaingia katika akademi hii.
Je, una maoni kwa hizi kelele zinazoendelea?
CC: @sifaelpaul
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments