JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUANZA OPERESHENI MAALUM KUWASAKA WATEJA WAO WANAODAIWA | ZamotoHabari.

 


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatoataarifa kwaUmma, kuwa kuanzia tarehe 14Juni 2021 litaanza Operesheni Maalum ya kuwasaka wateja ambao hawajafanya malipo yao kwenye Control numbers walizopewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. 

Tozo hizozipokwa mujibu wa Sheria namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na Kanuni ya Vyeti na Usalama wa moto ya Mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 (Fire and Rescue Force Safety Inspections and Certificates Regulations of 2008 GN.106 and its Amendment GN 63 of 2014). 

Pamoja na Kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya mwaka 2015 (Fire and Rescue Force Fire SafetyPrecaution in Building Regulations of 2015 GN 516).Jeshi linakusanya tozo (maduhuli)kwakufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwenye Majengo, Vyombo vyaUsafirishajiwa abiriana mizigo;na Usomaji wa ramani na michoro ya majengo.

 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linawatakawatejaambao hawajalipa nawalipewa Hati ya madai pamoja na Control numbers,wakalipe tozo hizokwenye Benki au kwa njia ya Mtandao wa Simukabla ya tarehe 14Juni, 2021 ili kuondokana na usumbufu utakao jitokeza. 

Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaokuwa hawajalipakwa wakati.Kwa huduma ya harakaya majanga ya moto na maokozi Piga namba 114.Imetolewa na;INSPJ. K. MwasabejaMsemaji Jeshi la Zimamoto na Uokoaj



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini