Maji ya chumvi yamsimamisha kazi Meneja RUWASA | ZamotoHabari.

  


Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amemsimamisha kazi aliyekuwa Meneja RUWASA wilaya ya Kongwa Mhandisi Hubert Kijazi, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Mkoka wilayani humo kuwa maji wanayoyatumia hayafai kwa matumizi ya binadamu kwa kuwa yana chumvi nyingi.

 

Waziri Aweso amefikia uamuzi huo wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa kisima ambao upo katika Kijiji hicho baada ya malalamiko ya wananchi na hivyo kutoa maelekezo ya kusimamishwa kazi kwa Meneja huyo ambaye kwa sasa ni Meneja wilaya ya Hanang ambapo hapo awali mradi wa kisima cha maji Mkoka ulikuwa chini yake na uligharimu shilingi milioni 600.


Waziri Aweso amesema maabara ambayo imetumika kupima maji hayo imeonesha wazi kuwa maji hayo yana chumvi nyingi hivyo hayafai kwa matumizi ya binadamu.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini