Maskini Huu Ndio Ugonjwa Uliopelekea Kifo cha Mchekeshaji Mzee Matata | ZamotoHabari.

 


Msanii wa maigizo ya vichekesho hapa nchini Tanzania Jumanne Alela maarufu kama Mzee Matata amefariki dunia jana saa 5:30 usiku katika Hospitali ya Muhimbili ambapo alilazwa tangu 13.6.2021.

 

Muigizaji mwenziye wa Tamthilia ya Mizengwe Mkwere original amesema Mzee Matata alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Kisukari kwa muda mrefu na mpaka umauti unamkuta chanzo kilikuwa ni ugonjwa huohuo.


Mkwere Original amesema kwa mujibu wa familia ya Mzee Matata,  msiba upo Chamanzi kwa Mkongo na mazishi yatafanyika kesho saa 7:00 Mchana kwenye makaburi ya Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini