Baada ya kuenea tetesi huenda Ajibu akarejea Yanga, baadhi ya mashabiki wameonesha kutotaka mchezaji huyo arejee kwa sababu aliondoka Yanga na kurudi Simba.
Kwa nini mashabiki wanataka kuwafanya wachezaji nao wawe kama mashabiki? Wachezaji ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine, leo anaweza kuwa kampuni hii kesho kampuni nyingine.
Ajibu alivyokuwa Yanga alifanya kazi yake kama ambavyo ilitakiwa na akaondoka kwenda sehemu nyingine baada ya kuona kuna maslahi mazuri. Kwa hiyo mtu akiondoka sehemu hatakiwi kurudi tena?
Kwa maisha ya soka mchezaji/kocha kuhama ni jambo la kawaida, asiye hama ni shabiki tu. Juma Kaseja amewahi kuhama Simba na Yanga zaidi ya mara moja.
Inawezekana wakati Ajibu anaondoka Yanga ilikuwa ni kipindi ambacho mashabiki wanamuhitaji, lakini hakuondoka vibaya hakufanya dharau wala kebehi zaidi naona aliangalia maslahi ya kazi yake kwa hiyo ukimlaumu sioni kama ni kitu kizuri.
Ajibu ni mchezaji mzuri, kama benchi la ufundi la Yanga linaona ni mchezaji atakayewasaidia sioni haja ya mashabiki kuweka presha. Waache akafanye kazi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments