Na Pamela Mollel,Arusha
Chuo cha uhasibu Arusha (IAA) kimezindua mitaala ya kufundisha Shahada ya usalama mtandaoni utakaoshirikiana na taasisi pont check ya nchini Israel.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo mkuu wa kitengo cha "Informatics" Allan Msolla alisema ushirikiano na taasisi hiyo utaongeza chachu kwa wanafunzi kujifunza kimataifa zaidi.
Waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari Dkt. Faustine Ndugulile aliyezindua mitaala hiyo alisema Dunia inabadilika kwa kasi na IAA wameliona hilo mapema hivyo anawapongeza.
"Suala la ajira limekuwa tatizo, si Tanzania pekee bali Duniani kote na kwa ubunifu nilioushuhudia hapa ni wazi wanaweza kujiajiri kupitia mitandao na kuajiri wengine" alisema Ndugulile.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Prof. Eliaman Sodoeka alisema ushirikiano wao na taasisi ya check point utawafanya wanafunzi wanaomaliza hapo kuwa sawa na wanafunzi wanaomaliza chuo chochote Duniani kwani taasisi hiyo inaaminika kimataifa kwa masuala ya ulinzi wa mitandao.
Naye Rais wa serikali ya wanafunzi IAA Sunday Kathbet anayekaribia kuhitimu alisema anatamani kurudia shule ili mambo mazuri yanayojitokeza hivi sasa na yeye afaidi, huku akiwasihi wanachuo wenzake kukitangaza vyema chuo hicho.
Hata hivyo mbali na uzinduzi huo wa mitaala lakini waziri alipata fursa ya kuzindua maabara ya TEHAMA katika shule ya sekondari Njiro iliyowezeshwa na IAA pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Arusha.
Picha ya pamoja kati ya uongozi wa IAA na walimu wa shule ya Sekondari Njiro Mara baada ya uzinduzi wa maabara ya TEHAMA shuleni hapo
Waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari Dkt Faustine Ndugulile akikagua komputa mara baada ya kuzindua maabara ya TEHAMA katika shule ya sekondari Njiro
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments