WAMI/RUVU yasisitiza Nishati Mbadala, Kuhifadhi Vyanzo vya Maji | ZamotoHabari.

Walimbwende wanaoshiriki Mashindano ya Miss Dodoma 2021 wakiwa wapozi kwa picha ya Pamoja na Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami / Ruvu, Baada ya Kutembelea Banda hilo na Kujifunza Mambo mbalimbali kuhusiana na Shughuli za Bodi hiyo kwenye Usimamizi wa Rasilimali za maji.


Machapisho mbalimbali yanayoelezea kwa kina kuhusiana na Rasilimali za maji na umuhimu wake, ambayo yanapatikana kwenye banda la Bodi ya Maji Bonde la Wami / Ruvu.

Mhandisi wa Rasilimali za Maji wa Bodi ya Maji Bonde la  / Wami / Ruvu akitoa Elimu kwa Wananchi mbalimbali kuhusu umuhimu wa Kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji ambao wamefika Kwenye Banda la Bodi hiyo katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Mjini Dodoma, ambapo yanafanyika Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani.
Mhandisi wa Rasilimali za Maji wa Bodi ya Maji Bonde la Wami / Ruvu, John Kassambili akielezea Umuhimu wa kutunza Mazingira hususani kwenye vyanzo vya Maji, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Mjini Dodoma, ambapo yanafanyika Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani. WAMI/RUVU yasisitiza Nishati Mbadala ili Kulinda na Kuhifadhi Vyanzo vya Maji 

Kuelekea Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, ambayo huadhimishwa kila ifikapo June 5, Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeelezea kujikita hasa kwenye kuihamasisha Jamii kuhusiana na Suala zima la Utunzaji wa Mazingira Kwenye Vyanzo vya Maji.

Imesema pamoja na Msisitizo huo, itaendelea kutoa Elimu kwa Makundi mbalimbali ya Wananchi kuhusiana na Matumizi ya Nishati Mbadala ikiwemo Gesi ama Nishati Banifu.

Mhandisi wa Rasilimali za Maji wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu John Kassambili akizungumza Wakati wa Maonesho ya Wiki ya Mazingira inayofanyika Mjini Dodoma kwenye Viwanja vya Jakaya Kikwete, amesema matumizi ya Nishati Mbadala yatasaidia Kupunguza Uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo mbalimbali vya maji ama Rasilimali za maji.

“Ukataji wa miti hovyo ni miongoni mwa viashiria hatarishi kwenye suala la utunzaji wa mazingira kwenye vyanzo hivyo vya maji, ambapo matumizi ya nishati mbadala ndio tiba sahihi ya kuendelea kutunza na kuimarisha rasilimali za maji” alisema Mhandisi Kassambili.

Kwa Upande wake Bwana Mashaka  Amrilok ni miongoni mwa Baadhi ya Wananchi Waliotembelea kwenye maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani, akizungumzia  kuhusiana na Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira kwenye vyanzo vya maji, amesema Baada ya kutembelea Banda la Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu amekiri kuridhishwa na Elimu aliyoipata kuhusu Mazingira na Umuhimu wa Matumizi ya Nishati Mbadala katika mizania ya Uhifadhi Endelevu wa vyanzo vya maji.

“ Nimejifunza zaidi kuhusu namna Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inavyoshiriki katika kuangalia vyanzo vya Maji katika Mto Wami lakini pia katika Maeneo mengine ya Mikoa Mbalimbali nchini ikiwemo wanavyofanya Tathmini ya Maji yaliyoko Chini ya Ardhi na Juu ya Ardhi”.

Maonesho ya Wiki ya Mazingira yanaendelea mjini Dodoma na yakitarajia kufikia kilele chake June 5, huku yakibeba Kauli mbiu inayosema Tutumie  Nishati Mbadala ili kuongoa Mifumo Ikolojia.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini