WATENDAJI WA SERIKALI WATAKIWA KUHAKIKISHA MIRADI YA MAENDELEO INAMALIZIKA KWA WAKATI | ZamotoHabari.


Woinde Shizza , Michuzi Tv-Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka watendaji wa serikali kuhakikisha miradi yote ya maendeleo ambayo serikali imetoa fedha zake inamalizika mapema na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Maelekezo hayo ameyatoa baada ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Karatu.

Amesema ni aibu miradi kutokamilika kwa wakati na kushindwa kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi, kwani fedha hizo ni kodi za wananchi.

" Nataka miradi hii isimamiwe kwa umakini mkubwa na ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma stahiki kwa wananchi."

Aidha, amewasihi watendaji wa serikali kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano kwani maendeleo yanaletwa kwa kuwa na nguvu ya pamoja.

Pia, amesisitiza kuwa hatavumilia jambo lolote ambalo halitafuata Sheria, taratibu na mfumo katika uongozi wake.

RC Mongella amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Karatu ambapo amekagua ujenzi wa Majengo mbalimbali ikiwemo kituao cha afya Endabush na Madarasa ya shule ya Sekondari Florian.

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella akikagua kituo cha afya Endabush kilichopo Wilayani Karatu Mkoani Arusha juzi alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani humo (picha na Woinde Shizza , ARUSHA)


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini