DC MPOGOLO ATOA SIKU SABA KWA WENYEVITI WA VIJIJI KUTATUA CHANGAMOTO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA | ZamotoHabari.

MKUU wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo ametoa siku saba kwa Viongozi wa Vijiji na Vitongoji kutatua kero ya migogoro Kati ya wakulima na wafugaji badala ya kuachia mamlaka zingine na kuonyesha si jukumu yao.

Mpogolo amelazimika kutoa maagizo hayo baada ya kukutana na utitiri wa migogoro hiyo akiwa Katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua Katika Kata za Ruvu na Njoro Wilayani humo.

Mpogolo amesema hayo Julai 27 na 28 katika Kata za Ruvu na Njoro Wilayani Same ambapo kukosekana kwa mahusiano na uwajibikaji wa viongozi hao wa ngazi ya chini kumepelekea mlundikano mkubwa wa kero za wananchi hao wa jamii za kifugaji na wakulima.  Amesema ndani ya siku Saba viongozi hao wawe wameshamaliza kusikiliza malalamiko hayo, kujadili na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kwa muda gani; na yeye atashiriki katika kikao cha WDC kitakachopokea Mapendekezo ya kila Kijiji.

Akiwa Katika ziara yake katika Kata hizo za Ruvu na Njoro Wilayani Same Mkuu huyo wa Wilaya amekutana na kero mbalimbali kutoka kwa wananchi hao huku migogoro Kati ya wakulima na wafugaji na uvamizi wa Tembo ikionekana kupamba moto zaidi na wakulima wakililia kuchungiwa mazao yao.









 

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini