Jeff Bezos na wenzake walitumia dakika 11 tu kwenda angani na kurejea | ZamotoHabari.


Bilionea Jeff Bezos amefanya ziaraa fupi kwenda angani, katika safari ya kwanzaa roketi yake, mpya, New Shepard.



Walisafiri kwa kutumia chombo kilichokuwa na madirisha makubwa yaliyowapatia nafasi ya kujionea picha za kuvutia za duniani.

Chombo hicho kilipotua baada ya safari ya zaidi ya dakika 10, Jeff Bezos alismea kwa furaha: “Siku bora zaidi!”

 

Chombo hicho kipya, kilichotengenezwa na kampuni ya Bezos ya Blue Origin, kimeundwa kuhudumia soko maalum la watalii wa angani.

Mwanzilishi wa Amazon Bezos – na washirika wengine katika “mbio za mabilionea kwenda angani” – wamekosolewa kwa kupeana kile ambacho kinaonekana kuwa safari ya kujivinjari kwa watu matajiri zaidi.

Wakosoaji wanasema fedha wanazotumia zingelitumiwa kuwaongeza mishahara wafanyakazi au kuimarisha juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo, Bw. Bezos inasisitiza maono ya mazingira: “Tunahitaji kupeleka viwanda vya shughuli nyingi, na tasnia yote inayochafua mazingira inastahili kupelekwa angani , ili tulinde sayari hii nzuri ya dunia,” aliiambia MSNBC.

“Itachukua miongo kadhaa kufikia lengo hilo, lakini lazima tuanze kwa hatua ndogo… ndivyo ujumbe huu wa utalii wa anga za mbali unatuwezesha kufanya, inatuwezesha kufanya mazoezi mara kwa mara.

Kuanzia kushoto: Mark Bezos, Jeff Bezos, Oliver Daemen, Wally Funk
,Kuanzia kushoto: Mark Bezos, Jeff Bezos, Oliver Daemen, Wally Funk
Bi Funk ndiye alikuwa mtu mwenye umri mkubwa kusafiri angani- na mdogo alikuwa mwanafunzi Oliver Daemen.

Chombo hicho kiliondoka saa 14:12 BST (09:12 EDT) kutoka eneo la uzinduzi wa kibinafsi karibu na Van Horn, Texas.

Baada ya ziara hiyo, Jeff Bezos alisema: “Matarajio yangu yalikuwa makubwa na yamekuwa makubwa na yalizidi sana”

Dakika mbili baada ya safiri, chombo hicho kilitengana na roketi yake na kuendelea mbele kuelekea laini ya Karman Line -mpaka unaotambuliwa zaidi angani,ambayo iko kilo mita 100 juu. Wanaanga hao wapya walipiga kelele wakisema “wow!” na kushangilia.

Wakati chombo kilipotua katika jangwa la Texas magaharibi
Wakati chombo kilipotua katika jangwa la Texas magharibi
Jeff Bezos alisema alishangazwa na hisia za microgravity: “Ilikuwa ya kawaida sana,” alielezea.

Bi Funk aliongeza: “Ilikuwa safari njema, Nilifurahia, Natamani sana kurejea tena.”

Katika miaka ya 1960, Bi Funk alikuwa mmoja wa kundi la wanawake waliofahamika kama Mercury 13.

Walipata vipimo sawa vya uchunguzi kama wanaanga wa kiume, lakini hawakupata kuruka chini ya mpango wa nafasi ya kitaifa ya Marekani.




APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini