KAMPUNI YA MURIYA YA NCHINI OMAN WAKUTANISHA WADAU SEKTA YA UJENZI NCHINI TANZANIA KUJADILI FURSA ZILIZOPO | ZamotoHabari.

 

WADAU mbalimbali katika tasnia ya ujenzi nchini Tanzania wamekutana kupitia onesho maalum ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Muriya yenye makazi yake nchini Oman, ambao ni wasanifu majengo ambapo pamoja na mambo mengine watajadiliana kwa upana fursa za uwekezaji zilizopo katika nchi ya Oman.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo ni kwamba onesho hilo hufanyika kila mwaka na safari hii litafanyika visiwani Zanzibar katika Hoteli ya Verde.Onesho limeanza jana Julai 28 hadi Julai 31, na kisha litafanyika jijini Dar es Salaam, katika Hoteli ya Sea Cliff, kuanzia Agosti 4 hadi 6 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa  moja jioni.

Imeelezwa kwamba wadau hao wataangalia mahitaji ya sasa ya soko na kutambulisha majengo mapya ya utalii yanayomilikiwa na Kampuni ya Muriya (ITCs) huko Oman pamoja na biashara ya makazi (real esate).

Wakati wa maonesho hayo, timu ya Muriya itaonyesha maendeleo bora ya makazi na fursa za uwekezaji wa kimataifa katika maeneo yake mawili ya makazi ambayo ni Jebel Sifah na Hawana Salalah, na kuzindua makazi yake mapya na eneo mpya ya burudani kwa maeneo yote mawili.

Kwa lengo la kuimarisha hadhi ya nchi ya Oman kama eneo muhimu la uwekezaji wa makazi ulimwenguni, hafla za maonesho ya Muriya zitaonesha mtiririko wa hotuba, mawasilisho, mazungumzo ya wataalam, na uchambuzi wa soko la makazi hayo.

Kutoka kwenye vyumba hadi majengo marefu ya kifahari (ghorofa) katika jamii zilizoendelea miradi inayotafutwa zaidi ya Muriya kote nchini Oman inaihakikishia mapato bora kuanzia $133,000, hii ni pamoja na makazi ya wanunuzi na familia zao.

Jebel Sifah, mradi wa makazi yaliyoko dakika 40 kutoka mji mkuu wa Muscat yapo eneo lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya milioni 6.2.Ina nyumba za makazi, ambazo ni za kumiliki au kukodisha, sehemu za maegesho ya boti binafsi 84, sehemu za vituo vya kulia na vya kupumzika, pamoja na uwanja wa gofu uliotengezwa na Mhandisi wa viwanja vya gofu maarufu duniani Peter Harradine.

Jebel Sifah, ni eneo lisolokuwa na msongamano wa watu Mjini Muscat, hutoa fursa ya uwekezaji wa aina moja ya kumiliki nyumba katika eneo lililotengenezwa vizuri, pia hukupatia fursa za makazi ya kuvutia zinazokuwezesha kucheza gofu, kufanya utalii wa bahari na kuangalia milima kwa uzuri zaidi.

Pamoja na eneo la ukubwa wa mita za mraba milioni 13.6, kivutio kikuu cha makazi ya Muriya Hawana Salalah yaliyopo katika jiji la kitropikana la Salalah katika mkoa wa Kigavana wa Dhofar, Oman.

Yalipo makazi hayo ndipo inakopatikana hifadhi ya kwanza ya maji nchini Oman ya Hawana, maegesho ya boti binafsi 170, makazi ya bure na kumbi za rejareja, migahawa na hoteli.

Makazi ya Hawana Salalah hulifanya eneo hili kuwa na nyumba na fursa za uwekezaji.

Kila mkazi katika eneo la Hawana Salalah hufurahia mandhari nzuri ya bahari, na imejengwa kwa kuzingatia, kuangalia na kuambatana na mitindo anuwai ya maisha, saizi ya chumba kimoja au viwili vya kulala, nyumba za mijini, majengo ya kifahari yaliyotengwa peke yake na majengo ya kifahari yaliyopo pwani ya bahari.

Pamoja na uwekezaji zaidi $ 750 milioni, Muriya wako nyuma ya maendeleo makubwa katika eneo la kiutawala la Sultan wa Oman na wataendelea kuleta maonesho ya makazi ambayo yanawakilisha fursa za kipekee za kuishi na uwekezaji.
Pichani kushoto ni Meneja mauzo kampuni ya Muriya Bi. Ghizlane El Gouchi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa onesho la kila mwaka la Mali nchini Tanzania ambalo limefanyika jana Julai 28,2021 katika ‘Hotel Verde’ , Zanzibar na litaendelea hadi Julai 31, na baadae kuendelea jijini Dar es Salaam, ‘Sea Cliff hotel’, kuanzia Agosti 4 hadi 6 ,2021.

Pichani kushoto ni Meneja mauzo kampuni ya Muriya Bi. Ghizlane El Gouchi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa onesho la kila mwaka la Mali nchini Tanzania ambalo limefanyika jana Julai 28,2021 katika ‘Hotel Verde’ , Zanzibar na litaendelea hadi Julai 31, na baadae kuendelea jijini Dar es Salaam, ‘Sea Cliff hotel’, kuanzia Agosti 4 hadi 6 ,2021.
Baadhi ya wafanyakazi kutoka katika kampuni ya Muriya, Oman wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa ukifanyika na waandishi wa habari. Mkutano huo ulifanyika hotel Verde Zanzibar mapema jana na utaendelea hadi tarehe 31 mwezi Julai
Baadhi ya wana habari na wageni waliohudhuria katika mkutano wa ufunguzi wa maonesho ya makazi kutoka Oman na kampuni ya Muriya wakiuliza maswali ili kufahamu zaidi kuhusu kampuni hiyo na manufaa yake kwa wananchi wa Tanzania watakaopata fursa ya kwenda kununua majengo na kuwekeza nchini Oman.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini