Na John Walter-Babati
Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ameyaomba mashirika binafsi yaliyomo wilayani humo kuendelea kuiunga mkono serikali katika kutoa elimu kwa Wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wimbi la tatu la UVIKO 19 na kutoa vifaa kinga katika maeneo hatarishi.
Ameyazungumza hayo leo julai 28,2021 akizungumza na NGOs ili kujua kazi zao na changamoto zinazowakabili,mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya mji wa Babati.
Twange amesema mashirika hayo kwa kuwa yanafanya kazi na watu yana nafasi katika kuhimiza wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na mlipuko wa ugonjwa huo.
Akieleza mikakati ya kujikinga na maradhi hayo, mkuu wa wilaya amesema wamejipanga kudhibiti mikusanyiko yote isiyokuwa ya lazima huku wataalamu wa afya wakiendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali.
Kwa upande wa mashirika hayo yameahidi kuendelea kuiunga mkono serikali ili kukabiliana na janga hilo la Korona kwa kuchukua tahadhari zinazopaswa wakati wote.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments