Sababu ya Waamuzi Simba Vs Yanga Kurudiwa Hii Hapa | ZamotoHabari.





KAMATI ya Waamuzi wa Ligi Kuu Bara, imeweka wazi sababu za kurudia majina ya waamuzi waliopangwa kuchezesha mchezo wa Kariakoo unaotarajiwa kupigwa leo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Orodha hiyo ambayo iliwekwa wazi juzi na Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB), ilionyesha kuwa waamuzi watakaochezesha mchezo wa kesho ni walewale ambao hapo awali walipangwa kuchezesha mchezo wa Mei 8, mwaka huu kabla ya mchezo huo kuahirishwa.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Soud Abdi Mohamed, alisema: “Kama Kamati tumeona hakuna haja ya kubadilisha waamuzi ambao walipangwa kuchezesha mchezo uliopangwa kuchezwa Mei 8, mwaka huu kabla ya kuahirishwa kutokana na sababu zilizokuwa zimejitokeza.“



Hii ni kwa sababu tayari maandalizi ya mchezo ule yalikuwa tayari yamefanyika, na kukamilika, tunaamini waamuzi waliokuwa wamepangwa watakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutimiza majukumu yao kwenye mchezo wa Jumamosi ya Julai 3, mwaka huu.

 

”Orodha kamili ya maofisa watakaosimamia mchezo Na. 208 wa Ligi Kuu ya Vodacom (Simba SC vs Young African SC) Julai 3, 2021 ni kama ifuatavyo;Kamisaa wa mchezo – Hosseah Lugano (Lindi) Mwamuzi wa kati – Emmanuel Mwandembwa (Arusha) Mwamuzi msaidizi namba moja – Frank Komba (Dar) Mwamuzi msaidizi namba mbili – Hamdan Saidi (Mtwara) Mwamuzi wa akiba – Ramadhani Kayoko (Dar) Mtathmini wa mwamuzi – Soudy Abdi (Arusha)Afisa mhusika – Jacquiline Kwamwamu (Dar)

STORI: JOEL THOMAS NA CAREEN OSCAR



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini