TRIPLE R&Z KUSINDIKIZA JUKWAA LA NANDY FESTIVAL | ZamotoHabari.


  Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

KUNDI la Triple R&Z Wanamuziki kutoka Taifa la Uingereza na Tanzania chini ya G Projects Tz wanaotamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo 'Moko moko'  wameonesha shauku yao ya kufanya kazi na msanii Faustine Mfinanga maarufu kama Nandy.

Triple R&Z wamebainisha hayo visiwani hapa walipokutana na Nandy kwa mara nyingine tokea wakutane nae kwa mara ya kwanza Desemba 2018 wakati wanaingia rasmi kwenye muziki.

"Wasanii wa Tanzania wote ni wazuri na kila mmoja tunampenda na kazi zao wote tunazifuatilia ila Nandy ni zaidi.

tungependa kufanya nae kazi hata wimbo mmoja ama zaidi" alisema Rehanna Nassor wa kundo hilo.

Rehanna ameongeza kuwa, Nandy ni miongoni mwa wasanii anaowasikiliza na pia kufuatilia shughuli zake za muziki ilikutimiza ndoto yake kimuziki.

"Role model wangu kwa wasanii wa nyumbani Tanzania namba moja ni Nandy.  
Natamani mafanikio yake kimuziki shauku yetu tufanye wimbo nae kama kundi tupo tayari" amesema Rehanna.

Triple R&Z walikuwa ni miongoni mwa wasanii wa muziki waliojumuika kumpokea Nandy alipowasili visiwani hapa kwa ajili ya shoo ya Nandy Festival itakayofanyika Uwanja wa Mao (Mau) siku ya Eid, kesho 21 Julai

Kundi hilo hadi sasa wana nyimbo zaidi ya Nane zikiwemo: Mommy and Dady, Zawadi, Kila kona, Good day, Hakuna matata, Tanzania raha na Moko moko.

Tayari Meneja wa Wasanii hao Gulu Ramadhani maarufu kama Dj G Lover ambaye pia Mkurugenzi Mkuu wa G-Recordz/Sharobaro Record  Tz amesema wanatatajia kuachia nyimbo mpya 3 kali zingine zikiwemo 'Kulandalanda'  Ice cream' na 'Birthday'.

Hata hivyo Dj G Lover kwa upande wake ameelezea kuwa, wataona namna ya Menejimenti yake na ya Msanii Nandy juu ya kufanya kazi.

Kundi hilo linaishi Uingereza ambapo kwa sasa wapo katika mapumziko mafupi nchini ikiwemo kufanya ziara kwa vyombo vya habari, kufanya shoo na kuandaa nyimbo hizo mpya katika studio tofautitofauti.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini