Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. ABUBAKAR KUNENGE amesema wataalamu wa Kilimo na Mifugo watapimwa kwa mikakati ya kuongeza uzalishaji.
RC Kunenge ametoa rai hiyo Julai 14, 2021 wakati akizungumza na Wataalamu wa Kilimo na Mifugo wa Ofisi yake kikao kilichoshirikisha Maafisa kutoka Benki ya Kilimo, Bodi ya Korosho na Kituo cha Utafiti TARI Nailiendele.
Kunenge ameeleza kutoridhishwa kwa hali ya uzalishaji wa mazao ya Kilimo na Mifugo, amewataka Wataalamu hao kuandaa Mikakati ya namna ya kusimamia mazao ya kilimo na mifugo ili kukuza uzalishaji. Amewataka Uongozi wote Mkoani hapo kusimamia Mikakati hiyo kila mmoja kwenye eneo lake.
"Nataka tujue tuko wapi na tunataka nini kwenye kilimo ili tusimamie na kutekeleza Mikakati ya kukuza uzalishaji na kupiga hatua. Ametaka Mikakati hiyo ipimike na atawapima Wataalamu hao kupitia utekelezaji wa Mikakati hiyo. Lazima tupimane alisisitiza Kunenge.
Amewataka wahusika wote kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo na mifugo kutekeleza na kusimamia Mikakati ya kukuza mazao. Ameeleza kuwa Wajibu Wananchi kwenye Kilimo cha Korosho kwa muda huu ni kusafisha mashamba, "wasafishe mashamba yao".
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA







0 Comments