Katika kumkomboa mtoto wa kike ili aweze kufikia malengo yake Shirika linapojishughulisha na masuala mbalimbali ikiwemo kutoa mikopo kwa wanawake, kutoa elimu ya miradi BRAC Maendeleo Tanzania limetoa vyeti kwa wanafunzi 86 ambao wamehitimu Mafunzo ya kozi fupi mbalimbali za ufundi stadi.
Mafunzo hayo yanayotolewa bure walengwa zaidi ni watoto wa kike ambao wamepata fursa kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Mapishi, urembo, Upambaji na ushonaji.
Akizungumza katika mahafali ya kuwatunukia vyeti wanafunzi hao, Mkurungezi wa BRAC International Afrika, Lucy Okowa amewataka wahitimu hao kutumia vyema Mafunzo waliyoyapata ili waweze kutimiza ndoto zao.
Okowa amesema wanafunzi hao wamenuafaika na Mafunzo hayo chini ya mradi wa Ela ambao umelenga kumyanyua mtoto wa kike na kumuwezesha kumudu maisha yake kiuchumi na kijamii na kufanikiwa kumaliza mafunzo na kupata msaada wa vifaa mbalimbali
Amesema wanawake duniani kote wamekuwa wakisifika kwa kuwa watu wenye ustahimilivu na kujitolea kwa nguvu zao zote katika kuhakikisha familia zao zinasonga mbele.
"BRAC ina amini kuwa ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuinua familia kwa ujumla ni muhimu kumwezesha mwanamke kwa sababu daima mwanamke hashindwi na jambo"amesema
Aliwasihi wahitimu hao wanapoanza safari ya ujasiriamali wawe makini ikiwa ni pamoja na kuzingatia Mafunzo mbalimbali waliyoyapata katika kipindi chote cha mafunzo.
"Ujasiriamali sio lelemama nawaomba muwe wavumilivu chagamoto nyingi mtapitia lakini msikate tamaa kila unapofeli nyanyuka, jifunze kutokana na makosa na uendelee kukaza mwendo kwa sababu wanawake sio jadi yetu Kushindwa"alisisitiza Okowa
Elina Patrick ni mmoja wa wanafunzi walionufaika na Mafunzo hayo katika eneo la Upambaji amesema Mafunzo aliyoyapata yatamsaidia kujikwamua na kujiajiri mwenyewe na kumuwezesha kupata kipato cha kumudu maisha yake.
"Matarajio yangu ni kufungua salooni yangu mwenyewe ambayo itanisaidia kutegeneza kipato changu mwenyewe "amesema
Naye Habiba Sangasi alilishukuru Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania kwa kumuwezesha kupata ujuzi uliokuwa ni ndoto yake katika maisha yake.
Mkurugenzi wa upande wa Africa wa BRAC International Bi. Ruth Okowa akikabidhi vifaa vya ujasiriamali kwa mmoja wa wasichana 86 ambao walipewa vifaa hivyo katika hafla iliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Temeke.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments