Pichani ni baadhi ya Watumishi wa BRELA wakisubiri kupatiwa huduma ya chanjo ya UVICO-19 katika hospitali ya Jeshi la Magereza, Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wakala wa usajili wa biashara na Leseni (BRELA) Agosti 13, 2021 wamejitokeza kwa wingi kupata chanjo ya Uviko- 19 katika hospitali ya Jeshi ya Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo ni muendelezo wa kuitikia wito wa Serikali unaowataka wananchi kujitokeza kwa hiari yao na kupata chanjo hiyo ya kujikinga na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Korona.
Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa akizungumzia zoezi hilo amesema ni muhimu kwa kila mtumishi kupata chanjo kuitikia maelekezo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema pia kwakuwa gonjwa hilo linahatarisha usalama wa wasiochanja ikiwa ni pamoja na watumishi, familia zao na jamii zinazowazunguka, siku zijazo kila mtumishi wa BRELA atapaswa kuchanjwa.
Kwa upande wa watumishi waliopata chanjo wamemshukuru Afisa Mtendaji Mkuu Bw Godfrey Nyaisa kwa kutoa usafiri na muda wa kazi kwa watumishi ili kwenda kupata chanjo hiyo.
Pichani ni baadhi ya Watumishi wa BRELA wakipatiwa huduma ya Chanjo ya UVICO -19 na Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Jeshi Ukonga, jijini Dar es Salaam, Bibi Rachel Mulamula.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments