Charles James, Michuzi TV
MBUNGE wa Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi ameishukuru Serikali kwa kuwezesha Jimbo lake kupatiwa mradi mkubwa wa maji wa kudumu wa Mto Udagaji ambao utagharimu kiasi cha fedha Sh Bilioni 3.7 ili kukamilika kwake.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mlimba, Kunambi amesema mradi huo wa maji utakwenda kumaliza kabisa kero ya maji ya muda mrefu ambayo imekua ikiwakabili wananchi wa Kata hiyo na vijiji vyake.
Kunambi amesema katika jitihada za kuhakikisha changamoto hiyo ya Maji inakwisha tayari Serikali imeshawaingizia kiasi cha Sh Milioni 600 za kuanza kwa mradi huo.
" Tunashukuru sana Serikali yetu kwa uwezeshaji wake kwetu kwenye mradi huu, hii inaonesha dhahiri ni jinsi gani Rais wetu Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwatua akina Mama Ndoo kichwani, kupitia mradi huu mkubwa Sasa Mlimba itakwenda kumaliza kero ya maji.
Kiasi kitakachogharimu mradi huu ni Sh Bilioni 3.7 mpaka Sasa Serikali ishatupatia Sh Milioni 600 na fedha hizi zimeshaanza kutumika kwa kukamilisha ujenzi wa eneo lile la chanzo cha maji na sasa wameagiza mabomba makubwa ya kutandika Kutoka Sasa Udagaji kuleta maji hapa Mlimba, " Amesema Kunambi.
Katika hatua nyingine Mbunge Kunambi amekabidhi kiasi cha Sh Laki Tano kwenye Shule ya Msingi Lumumwe kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo ambavyo vimeharibika.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi (katikati) akimkabidhi mtendaji wa Kijiji Cha Lumumwe kiasi cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa vyoo vya Shule ya Msingi Lumumwe Kata ya Kamwene.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali Kata ya Kamwene alipofika kukagua maendeleo ya miradi kwenye Kata hiyo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments