Mwanamke Mwenye Mdomo Mkubwa Zaidi Duniani | ZamotoHabari.





DUNIA hii tunayoishi ni kongwe kwelikweli kiasi kwamba kwa sasa ina umri wa zaidi miaka bilioni 4.5! Kwa ukongwe huo, utakubaliana na mimi kwamba imejaa simulizi nyingi za kusisimua na kushangaza.

 

Miongoni mwa simulizi hizo, ipo moja ya mwanamke anayeshikilia rekodi ya Kitabu cha Kumbukumbu za Dunia cha Guinness kwa kuwa na kinywa kikubwa zaidi duniani; Samantha Ramsdell.

 

Samantha amewaacha midomo wazi wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti video akionesha namna pakiti nzima ya vibanzi (crips) inavyoweza kuishia yote kwenye kinywa chake.

 

Video za Samantha zimeteka kwenye Mtandao wa TikTok na kuwashangaza wengi kutokana na ukubwa huo wa kinywa chake.

 

Kwa mujibu wa Samantha mwenyewe, waumiaji wa Mtandao wa TikTok walikubaliana kuwa anahitaji rekodi hiyo baada ya kutazama video zake akipanua kinywa chake na kumtaka ashiriki kwenye mchezo wa kutanua kinywa na kweli aliposhiriki akaibuka kidedea na kutajwa kama mwanamke mwenye kinywa kikubwa zaidi duniani.

 

Hivi karibuni, Samantha aliwashtua wafuasi wake kwa video yake akionesha namna pakiti nzima ya vibanzi inaweza kutoshea kinywani mwake kwa mkupuo mmoja.

 

Video yake ilichapishwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Televisheni ya CNN huku wanamtandao wakishtuka kuwa mrembo huyo anaweza kumeza chakula kizima wakati mmoja.

 

Maoni ya wanamtandao wa Twitter yalikuwa ni mengi huku kila mmoja akionesha kuduwazwa na baadhi wakitaka kujua kiasi ya chakula ambacho Samantha hula na kuhisi kushiba.

 

“Kama anaweza kula pakiti nzima kwa wakati mmoja, je, anahitaji pakiti ngapi ili aweze kushiba?” Alihoji mmoja wa watumiaji hao wa Mtandao wa Twitter.

 

Kwa mujibu wa Samantha, alitambua tangu akiwa mtoto kwamba ana mdomo mkubwa kutokana na picha zake za utotoni alizokuwa akioneshwa.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini