Mwanmuziki wa Hip Hop P Mawenge ameweka wazi ukweli wake juu ya uwezo wa Hamisa Mobetto kwenye Muziki ikiwemo kazi yake mpya Ex Wangu .
Mawenge amefunguka kwa kusema Hamisa Mobetto atulie kwenye Mitindo kwenye Muziki bado sana na akisisitiza sio lazima wote tuwe wanamuziki
" Wimbo wake mbaya sijui Hata Producer Kafanyaje lazima tuwe wakweli Sio lazima wote tuwe wanamuziki yeye akae kwenye uanamitindo muziki hawezi ni very poor artist kupata viewers haimaanishi wewe mkali unaweza kupata kutokana umaarufu wako - Amesema P Mawenge .
Mawenge amemalizia kwa kusema akipigwa msasa akiwa bora atasema ila kwa sasa bado
Unakubaliana na P Mawenge ?
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments